Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko MCT yashauri waandishi kujiunga JOWUTA
Habari Mchanganyiko

MCT yashauri waandishi kujiunga JOWUTA

Rais wa MCT, Jaji mstaafu Juxon Mlay
Spread the love

 

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limewashauri waandishi wa habari nchini kujiunga na Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), ili waweze kupigania maslahi yao kwa pamoja. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na Rais wa MCT, Jaji mstaafu Juxon Mlay wakati akifunga Mkutano Mkuu wa 23 baraza hilo uliofanyika kwa njia ya mtandao jana Alhamisi, tarehe 30 Oktoba 2021.

Jaji mstaafu Mlay alisema kwa muda mrefu MCT ilikuwa inatamani kuona chama cha kupigania na kulinda maslahi ya waandishi wa habari hivyo ujio wa JOWUTA ni muhimu kwa tasinia hiyo.

Alisema waandishi ni kundi muhimu katika kupigania haki, uhuru, amani, maendeleo, uchumi, huduma za jamiii na mambo mengine hivyo wanapaswaku katika chombo kimoja kufanikisha hayo.

“Nichukue nafasi hii kuwapongeza wote waliofanikisha uanzishwaji wa JOWUTA na wanachama waliopo sasa. Nitumie mkutano huu wa 23 wa MCT kuaomba waandishi wote Tanzania kujiunga na chama hiki kwani ni sehemu sahihi katika kudai maslahi yetu,” alisema.

Rais huyo wa baraza alisema, pamoja na kuwepo kwa sheria ya huduma za habari sehemu sahihi ya kudai maslahi ya waandishi ni JOWUTA kwa kuwa ni chombo kinachotambulika Serikalini.

Aidha, Jaji mstaafu Mlay ameweka wazi kuwa atahakikisha MCT inashirikiana na JOWUTA katika kufanikisha malengo yake.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga

Akizungumzia mkutano Mkuu wa 23 wa MCT, Rais huyo alisema anaipongeza sekretarieti kwa kufanikisha kufanyika na kutekeleza mipango yake pamoja na changamoto ya Uviko-19.

Alitumia mkutano huo kuwaasa waandishi wa habari kutumia kalamu zao kwa kuandika habari zenye tija na nchi na wananchi.

“Waandishi niwaombe mtumie kalamu zenu viziru ili kusaidia nchi msikubali kutumika. Tumuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwani ameonesha nia njema dhidi yetu,” alisema.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alisema ujio wa JOWUTA ni mwanga kwa tasnia ya habari ambayo imgawanyika hivyo anaungana na Rais kuwaomba na kuwashauri waandishi kujiunga nayo.

Kuhusu mkutano huo wa mwaka wa MCT alisema umekuwa wa mafanikio mazuri huku akisisitiza wanachama kulipa ada ili kujenga baraza imara.

Alisema MCT imefanikiwa kupata ofisi yake katika eneo la Tegeta pamoja na kutekeleza mapendekezo ya mkutano mkuu wa 22 uliofanyika jijini Tanga mwaka jana.

Mukajanga alisema baraza linaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali na Serekali kuhakikisha sheria zisizo rafiki na tasnia hii zinaondolewa.

“Mkutano wetu ulikuwa na ajenda 10 zimepitiwa zote na kukubalika sasa tunajipanga kutekeleza mwaka mpya wa fedha kwa waledi, uadilifu na uaminifu ili kusukuma gurudumu hili mbele,” alisema

Kupitia mkutano huo Kajubi alipitishwa na wanachama kuendelea kuwa Katibu Mtendaji wa MCT kwa kipindi kingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

error: Content is protected !!