Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mchungaji Zimbwabwe yamkuta ya Lema
Kimataifa

Mchungaji Zimbwabwe yamkuta ya Lema

Patrick Mugadza, Mchungaji na mtetezi wa Haki za Binadamu nchini Zimbabwe
Spread the love

PATRICK Mugadza, Mchungaji na mtetezi wa Haki za Binadamu nchini Zimbabwe ametupwa ruamnde baada ya kutabiri kifo cha Rais Robert Mugabe wan chi hiyo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Mugadza alidai kuwa akiwa kwenye maombi Disemba 26 mwaka jana Mungu alimwambia kuwa, Oktoba 17 mwaka 2017 itakuwa siku ya kifo cha Rais Mugabe.

Gift Mtisi mwanasheria wa Mchungaji huyo amethibitisha kukamatwa kwa mteja wake ambapo amesema Jeshi la polisi Kitengo cha Makosa ya Jinai kinamhoji kutokana na utabiri wake.

“Ni kweli amekamatwa na polisi lakini hatuna taarifa zaidi kwa sasa ingawa tunajua atakuwa anahojiwa kutokana na tukio hilo lililojiri mwaka jana,” alisema Mtisi.

Itakumbukwa kuwa Godbless Lema Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anashikiliwa katika gereza la Kisongo mkoani Arusha kwa miezi miwili sasa, baada ya kudai ameota ndoto kuwa Rais John Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 iwapo ataendelea na kiburi.

Ingawa mahakama haijampata na hatia lakini hajapewa dhamana mpaka sasa kutokana na mvutano uliopo baina ya mawakili wa upande wa mshitakiwa na upande wa serikali, huku kesi hiyo ikiendelea kupigwa kalenda mara kwa mara.

Mchungaji Mugadza wa Zimbambwe, wakati akitoa utabiri kuwa Rais Mugambe atakufa Oktoba mwaka huu alisema hafurahii kifo hicho lakini inampasa kutangaza utabiri huo kwasababu ni maono aliyofunuliwa na Mungu.

“Si kwamba nafurahi kutangaza hili lakini nalazimika kusema kile ambacho Mungu alinionesha Disemba 26 pale nilipokuwa kwenye maombi. Oktoba 17, 2017 Rais Mugabe atakufa,” alinukuliwa akisema mchunganji huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!