August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mchungaji Nyaga atoa Sh. 10 mil. kwa masikini

Mchungaji Nyaga akigawa mifuko ya unga

Spread the love

PETER Nyaga, Mchungaji wa Kanisa la RGC Tabata Chang’ombe, ametoa misaada inayogharimu kiasi cha Sh. 10 milioni kwa watu wasiojiweza na wanaoishi katika lindi la umasikini, anaandika Aisha Amran.

Mchungaji huyo  ametoa misaada hiyo kwa watu 600 kutoka maeneo ya Tabata Chang’ombe wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kanisa la R.G.C Tabata Chang’ombe.

Misaada iliyotolewa ilielekezwa kwa wajane, wagane, yatima, watu wasiojiweza na wenye ulemavu wa ngozi, huku mchungaji Nyaga akisema, “miongoni mwa watu hao, wapo watu 80 wenye ulemavu wa ngozi ambapo kila mmoja amepata unga kilo tano, mwamvuli, sabuni, miswaki, dawa pamoja na Sh. 400,000/= ya nauli.”

Ameongeza kuwa, “hata watu wengine nao  wamepata sabuni, unga kiroba kimoja cha kilo tano ili nao wapate kufurahi pamoja na kanisa linalotimiza miaka 10 hivi sasa nchini.”

Nyaga amesema, utoaji huo wa misaada kwa makundi yasiyojiweza hufanyika kila mwaka huku akitoa wito kwa wachungaji wengine kuiga mfano wake wa kusaidia masikini.

Kwa mujibu wa mchungaji huyo  anasema katika kazi za kiroho kwa muda wa miaka 10, wamefanya mikutano 170 na kukoa watu zaidi ya 450,000 ikiwemo kufungua matawi ya makanisa 10.

Mchungaji huyo alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kudumisha amani ikiwa ni pamoja na wale wenye uwezo wa kuwasaidia wasiokuwa nacho.

error: Content is protected !!