Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mchungaji Msigwa: Sioni wa kunishinda Iringa Mjini
Habari za Siasa

Mchungaji Msigwa: Sioni wa kunishinda Iringa Mjini

Mch. Peter Msigwa, Mtia nia wa ubunge jimbo la Iringa Mjini akijinadi mbele ya wapiga kura
Spread the love

MBUNGE anayemaliza muda wake wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa ameshinda kura za maoni kutetea nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa…(endelea)

Mkutano wa kura za maoni jimbo la Iringa Mjini umefanyika leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020 na kusimamiwa na Fanuel Mkisi ukiwa na wagombea wane na sita wa viti maalum.

Akitangaza matokeo hayo, Mkisi amesema, Mchungaji Msigwa amepata kura 117 kati ya kura 131 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano huo akifuatiwa na Pallaiga Mlasu kura 13.

Wengine ni Aidan Salehe ambaye amepata kura 0 na Frank Nyalusi kura 1.

Upande wa viti maalum, Mkisi amesema Suzan Mgonokulima ambaye amepita kwa kura 31. Suzan ni mbunge anayemaliza muda wake wa viti maalum.

Amesema, Celestina Kokombay amepata kura 17, Rose Chumi 12, Anastazia Mwamongi 0, Aida Mbilinyi nane na Theodora Kalumwanga 2.

Baada ya kutangwa mshindi, Mchungaji Msigwa amesema yeye yupo kutetea masilahi ya Wanairinga.

Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa mjini

Mchungaji Msigwa ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka kumi mfululizo amewashuruku wajumbe kwa kumuamini na atahakikisha anapigana kutetea jimbo la Iringa Mjini libaki kuwa la Chadema.

Aidha amesema, hajaona wa kushindana nae katika jimbo hilo hivyo anauhakika na anatoka katika ukumbi huu akiwa na jeuri ya kukutana na yeyote kutoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika kura za maoni za CCM, Jesca Msambatavangu aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Iringa ndiye aliongoza na anasubiri vikao kuamua ama awe yeye au mwingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!