April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

 Mchungaji Msigwa awavaa wanaoikosoa Chadema

Mch. Peter Msigwa

Spread the love

MCHUNGAJI Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini amewashukia wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wanao kikosoa chama hicho mitandaoni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kupitia ukurasa wake wa Twitter leo tarehe 16 Desemba 2019, Mchungaji Msigwa amewashauri wafuasi wa Chadema wenye maoni juu ya chama hicho, kupeleka ushauri wao kwenye vikao vya chama.

Mwenyekiti huyo wa Chadema Kanda ya Nyasa, amewashangaa wanachama hao wanaoshindwa kufikisha ushauri wao katika vikao vya chama, na badala yake wanapeleka madukuduku yao mitandaoni.

“Kuna vikao ambavyo vinaanzia kwenye msingi kwa sisi Chadema, mpaka taifa. Sasa wewe kama ni Mwana Chedema, kama una ushauri anzia huko.

Lakini wengi hawataki kuhudhuria huko , ila kwenye mitandao ndio mafundi wa kukosoa. Chama lazima kiwe na nidhamu, Chama ni vikao, lazima tuheshimu,” ameandika Mchungaji Msigwa.

error: Content is protected !!