Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mchungaji Msigwa amwomba msahama Kinana
Habari za Siasa

Mchungaji Msigwa amwomba msahama Kinana

Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini
Spread the love

MCHUNGAJI Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), amemuomba radhi Abdulrahman Kinana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kumhusisha na biashara ya ujangili na uuzaji wa nyara za serikali. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Mchungaji Msigwa ameomba msamaha huo leo Jumanne tarehe 19 Mei, 2020 jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari huku akisisitiza, tuhuma hizo alizotoa dhidi ya Kinana mwaka 2013, hazikuwa za kweli.

Mchungaji Msigwa alitoa shutuma hizo bungeni jijini Dodoma akiwa waziri kivuli wa maliasili na utalii kwa wakati huo, wakati akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, katika mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo, kwa mwaka 2013/2014.

“Leo nakiri mbele yenu kwamba tuhuma hizo nilizotoa dhidi ya Kinana hazikuwa na ukweli wala ushahidi wowote, taarifa nilizotumiwa hazikuwa sahihi bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa.”

“Nasikitika hizo taarifa nilipewa na mtu niliyemwamini, kwa bahati mbaya hazikuwa za kweli,” amesema Mchungaji Msigwa.

Hatua ya Mchungaji Msigwa kutoka hadharani na kumuomba radhi, imetokana na Shauri Na. 108/2013, aliyofunguliwa na Kinana, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mwaka 2013.

Katika shauri hilo, lililokuwa linaendeshwa na Jaji Zainab Mruke, Mchungaji Msigwa alikutwa na hatia kutokana na kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya Kinana, mahakamani hapo.

“Kinana alinifungulia mashataka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Shauri Na. 108/2013, katika kesi hiyo iliyosikilizwa na kuhukumiwa na  Jaji Zainab Mruke, nilikutwa na hatia baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma zangu mbele ya mahakama,” amesema Mchungaji Msigwa.

Amesema licha ya kumuomba msamaha Kinana na kusamehewa,  ameamua kutoka hadharani, kwa kuwa makosa yake hayakumuumiza mwanasiasa huyo peke yake, bali yaliiumiza familia yake, na jamii inayomzunguka.

“Ni dhahiri kauli zangu dhidi yake nilimkosea, nilimkasirisha na kumkashfu Mzee Kinana, nafurahi nimekutana nae na kumuomba radhi yeye binafsi na kukubali anisamehe.”

“Nimekuja hadharani kuomba radhi kwa kuwa, aliyeumizwa si Kinana peke yake bali ndugu zake na wanaomfahamu,” amesema Mchungaji Msigwa.

Amesema kujitokeza kwake hadharani kuomba radhi, hakumaanishi kwamba ni udhaifu bali ni kitendo cha kiungwana pale unapobaini kilichosemwa, hakina ukweli wowote hivyo unapaswa kuomba radhi.

Mchungaji Msigwa amesema viongozi mbalimbali waungwana wamekuwa wakiomba radhi pindi wanapobaini wamekosea, lakini kiongozi anayekosea na hakubali makosa, huyo hafai kuwa kiongozi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!