
Mchungaji Peter Msigwa
ALIYEKUWA Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, amemtuhumu Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, alikuwa “wakala wa mradi wa ununuzi wa wabunge wa upinzani.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Amesema, “niliwahi kuitwa na Spika Ndugai na kuelezwa kuwa amepewa ujumbe na Rais Magufuli (Dk. John Pombe Magufuli), kwamba nijiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama ninataka kurudi tena bungeni. Lakini nilimkatalia.”

Msigwa ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, amesema kuwa Ndugai aliwahi kumwita ofisini kwake na kumshawishi ajiunge na CCM.
Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema la leo Ijumaa, tarehe 18 Juni 2021, kujua pia alichokijibu Spika Ndugai kuhusu tuhuma hizo.
More Stories
Huduma ya Teleza Kidigitali yazinduliwa Morogoro
Taasisi yaanzisha mafunzo kuwanoa wadau wa mawasiliano nchini
GGML yatoa msaada wa magari manne VETA Mwanza