Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchungaji atoa neno ‘watu wasiojulikana’
Habari Mchanganyiko

Mchungaji atoa neno ‘watu wasiojulikana’

Michael Nhonya akifundisha somo la Uongozi kwneye Kongamano la Vijana Taifa June, 2017
Spread the love

KANISA la Wabaptist Tanzania limewataka viongozi wa serikali pamoja na vyama vya siasa kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa kulinda amani ya nchi, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo limetolewa huku kukiwa na wimbi la kuwapo matukio mbalimbali ya uhalifu yakiwamo ya watu kuvamiwa na kupigwa risasi na ”watu wasiojulikana”

Makamu mwangalizi mkuu wa Kanisa la Wabaptist Tanzania (BCT) Mchungaji, Michael Nhonya, alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akihubiri katika ibada iliyofanyika kanisani hapo eneo la Makole mkoani Dodoma.

Amesema kuwa hali ya wasiwasi inayojitokeza kutokana na vitendo ambavyo vinavyoashiria kupoteza amani ni muhimu vyombo hivyo  vikasaidia kudumisha amani ya nchi.

Amesema ili kukabiliana na vitendo hivyo visiendelee kujitokeza kuna haja ya serikali kuingilia kati na kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini wahalifu hao.

Amesema kuwa  kanisa hilo kamwe halitaweza kuvivumilia vitendo hivyo bila kuvikemea.
Ameongeza kuwa bado wanaamini nchi ya Tanzania ni ya amani na utulivu.

“Sisi kama viongozi wa dini tutaendelea kukemea kila mtu bila kujali cheo chake, tutasema na kuelekeza inapobidi kufanya hivyo”, amesema.

Amewataka  Watanzania kuwa na subira wakati vyombo vya dola nchini vikiendelea kuchunguza matukio yanayotokea kwa sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!