Saturday , 15 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchungaji amvaa Spika Ndugai
Habari MchanganyikoTangulizi

Mchungaji amvaa Spika Ndugai

Spread the love
MWANGALIZI wa Makanisa ya Baptist mkoani Dodoma, Antony Mlyashimba, amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kutubu na kisha kukaa meza moja na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad. Anaripoti Danson Kaijage kutoka Dodoma … (endelea).

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili, muda mfupi baada ya kumalizika ibada ya sikukuu ya kumbukumbu ya kufufika Yesu Kristo, Mchungaji Mlyashimba alisema, Bunge linapaswa kutumia siku ya Pasaka kujitathimini juu ya malumbano yake na Prof. Assad.

“Bunge haliwezi kukwepa kuitwa dhaifu; na kuendelea na malumbano dhidi ya Prof. Assad, ni dalili udhaifu huo na kutaka kuligawa taifa,” ameeleza.

Amesema, “ni vema Bunge na Spika wake Ndugai, wakatubu na kukaa meza moja na Prof. Assad ili kulinusuru taifa na migawanyuiko.

Alisema, hatua hiyo ndio yenye mafufaa na tija kwa taifa huku akiwaelekeza wabunge kujitafakari na kujiuliza sala yao wanayoisali kila siku asubuhi kabla hawajaanza vikao vya Bunge inawaelekezaje.

Mchungaji Mlyashimba amesisitiza kuwa mvutano unaoendelea kati ya CAG kwa cheo chake na Bunge kwa muhimili wake, ni kutaka kuligawanya taifa katika vipande viwili.

Kauli ya Mchungaji Mlyashimba imekuja siku moja baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), kumuandikia barua waziri mkuu wa Jamhuri, Kassim Majaliwa kumuomba kuingilia kati mvutano kati ya CAG na Bunge.

Katika barua yake ya 18 Aprili, LHRC inasema, hatua ya Bunge kutaka kujitenga na Prof. Assad, ni kutaka kuingiza nchi katika mgogoro wa kikatiba na kugoma kuwajibika kwa maslahi ya taifa.

Kituo hicho, kimemshauri Majaliwa, kulifikisha jambo hilo kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri na bungeni mjini Dodoma, ili kuangalia njia bora ya kutengua uamuzi huo.

Aidha, wito wa Mchungaji Mlyashimba, unakuja siku mbili baada ya Prof. Assad kusisitiza kuwa hayuko tayari kung’atuka kutoka kwenye wadhifa wake.

Taarifa zinazowanukuu watu waliokaribu na Prof. Assad zinasema, pamoja na kufuatwa na viongozi mbali mbali kumuomba kujiuzulu, kiongozi huyo, amegoma katakata kukubaliana na ombi hilo.

Mapema mwezi huu, Bunge lilipitisha azimio la kutokufanya kazi na Prof. Assad baada ya kumtuhumu kulidhalilisha kufuatia kauli yake aliyoitoa katika mahojiano yake nad Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York nchini Marekani, Desemba mwaka 2018.

Katika mahojiano hayo, Prof. Assad alisema, “Bunge la Tanzania limekuwa dhaifu na hivyo limeshindwa kuwajibisha serikali.”

Akizungumzia kauli hiyo ya Prof. Assad, MchungajiMlyashimba amesema, Bunge haliwezi kukwepa kuitwa dhaifu kwa kuwa hata vitabu vitakatifu vimesisitiza hakuna aliyemkamilifu.”

“Hili jambo tunatakiwa kulizungumza kama Wakristo na kama taifa. Bunge wanasema hawataki kufanya kazi na CAG, ambaye ni Prof. Mussa Assad; na CAG anasema, ‘Bunge ni dhaifu.’

“Sasa nataka niwakumbushe wabunge kila wanapoanza vikao asubuhi, wana sala yao ambayo kuna kipengele kinachosema, ‘Mungu tuongeze hekima na busara.’ Kama wangekuwa hawana mapungufu, wasingehitaji nyongeza wanayoomba,” ameeleza.

Amesema, “kwanza, niwashukuru wabunge wanatambua kuwa wanamapungufu na kuwa na mapungufu ni sawa na kuwa dhaifu. Kwa  maana hiyo, wanayo mapungufu na mapungufu hayo yanawapelekea kuwa na sala ambayo inawaelekeza kumwomba Mungu ili awaongezee hekima na busara.”

Aidha, mchungaji huyo ambaye pia ni mchungaji wa Baptist Makole mkoani Dodoma amesema, wabunge wanatakiwa kutubu na kutengua kauli au azimio lao la kutokutaka kufanya kazi na Pro. Assad.

Kiongozi huyo wa kiroho alisema, kitendo cha kuweka azimio la kutokufanya kazi na CAG ambaye ni macho ya kusaidia pale ambako i mambo hayaendi sawa, ni moja ya udhaifu.

Mchungaji huyo alisema, kwa sasa nchi imeingia katika marumbano ambayo hayana maana kutokana na mvutano kwa wanaounga mkono kauli ya CAG na wale wanaokubaliana na azimio la Bunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!