August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mchina adakwa kwa kuiba siri za Marekani

Spread the love

MTU mmoja raia wa China aliyefahamika kwa jina la Su Bin amekiri kuhusika katika njama za kuiba siri za mifumo ya ndege za kijeshi za Marekani, anaandika

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) limeeleza kuwa, Su Bin aliyekamatwa nchini Canada tayari amekiri kufanya kazi na watu wawili kutoka China kati ya Oktoba 28 na Machi 2014 kudukua mifumo ya Kompyuta ya Marekani ikiwemo Kompyuta ya Boeing inayotumiwa na Jeshi la Marekani kuunda ndege zake.

Hata hivyo Su Bin (50) anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba taarifa za kuhusu ndege za kubeba mizigo na silaha.

Amedaiwa kuwa na kampuni ya teknolojia ya uchukuzi wa ndege nchini Canada ambaye tangu mwaka 2014 amekuwa akitafuta uraia wa Canada bila mafanikio.

error: Content is protected !!