July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mchezo wa Azam FC dhidi ya Simba, wasogezwa mbele

Kikosi cha Simba kikifanya mazoezi

Spread the love

 

KUFUATIA kupata ajali mbaya ya gari, kwa kikosi cha timu ya Polisi Tanzania mkoani Kilimanjaro, bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesogeza mbele kwa siku moja michezo ya mzunguko wa 33, kutoka Julai 14 mpaka Julai 15, 2021, ikiwemo mchezo wa Azam FC dhidi ya Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa mzunguko wa pili sasa utapigwa tarehe 15 Julai, kwenye dimba la Azam Complex Chamazi.

Kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye dimba la Benjamin Mkapa, ambapo Simba walikuwa nyumbani tarehe 7 Februari 2021, timu hizo zilimaliza kwa sare ya mabao 2-2.

Taarifa kutoka bodi ya Ligi imeeleza kuwa, wameamua kuchukua hatua hiyo mara baada ya uongozi wa klabu hiyo kuomba kusogezea mbele mchezo wa wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.

Mzunguko huo wa 33 ulikuwa na michezo 11, ambayo ni Mbeya City dhidi ya Gwambina FC, Tanzania Prisons kuvaana na Biashara United, KMC kuwakabili JKT Tanzania, Yanga kuwaalika Ihefu FC, Dodoma Jiji dhidi ya Mtibwa Sugar, Coastal Union na Mwadui na mchezo wa mwisho ulikuwa Ruvu Shooting dhidi ya Namungo FC.

Kikosi hiko cha timu ya Polisi Tanzania, kilipata ajali tarehe 9 Julai, walipokuwa wakitoka kwenye mazoezi kwenye Uwanja wa PTC, na kurejea kambini.

Katika ajali hiyo, mshambuliaji wa kikosi hiko, Mathias Mdamu aliumia vibaya kwa kuvunjika miguu yote miwili, na kuendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya KCMC.

Afisa uhusiano msaidizi wa Hospitali hiyo Joel Masawe amesema kuwa, mpaka sasa mshambuliaji huyo aliyevunjika miguu alikuwa na hali mbaya, lakini wachezaji wengine 13, wanaendelea kupatiwa matibabu.

“Mshambuliaji Mdamu ambaye alivunjika miguu yote, yeye yupo kwenye hali mbaya, lakini wachezaji engine 13 wanaendelea kupatiwa matibabu.

“Dereva nae aliletwa akiwa amevunjika mbavu moja nae pia amelazwa akiwa anapatiwa matibabu zaidi,” alisema afisa mahusiano huyo.

Polisi Tanzania kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa na pointi 42, na ilikuwa iikijindaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao ulikuwa upigwe kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi.

error: Content is protected !!