Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mchezaji wa zamani wa Taifa Zambia, Kaizer Chiefs afariki kwa kushambuliwa na mbwa wake
Kimataifa

Mchezaji wa zamani wa Taifa Zambia, Kaizer Chiefs afariki kwa kushambuliwa na mbwa wake

Philemon Mulala
Spread the love

 

NYOTA wa zamani wa Chipolopolo, Philemon Mulala amefariki dunia baada ya kuumwa na mbwa wake watatu nyumbani kwake Lichtenburg Afrika Kusini. Yameripoti Mashirika ya Habari ya Kimatiafa … (endelea).

Taarifa zinaeleza kuwa Mulala aliumwa na mbwa hao alipotoka nje kuchunguza kwanini walikuwa wanabweka sana baada ya umeme kukatika.

Msemaji wa polisi, Sam Tselanyane, ameiambia BBC kuwa mke wake aliwaambia kwamba alisikia mbwa wakibweka lakini hakujishughulisha na kwenda kuangalia ni nini kilikuwa kibaya kwani mbwa hao mara kwa mara walikuwa wakiwabwekea watembea kwa miguu na magari yaliyokuwa yakipita.

“Baada ya umeme kurudi, aliingia ndani ya nyumba hiyo akimtafuta mumewe lakini hakumpata, baada ya kuendelea na upekuzi, mwanamke huyo alimuona mumewe akiwa amelala nje kwenye bustani. Kisha akatoka nje kupeleleza kulikoni, na akagundua mume wake alikuwa hatikisiki baada ya kuumwa na mbwa wao watatu.”

Mamlaka zimewaondoa mbwa hao wawili ambao ni ‘Cross breed” ya Pitbul na mbwa wa tatu hajulikani asili yake ila anasemekana kuwa mkali.

Mulala alihamia Afrika Kusini kuichezea klabu ya Kaizer Chiefs mwaka wa 1988. Pia alichezea Cape Town Spurs na Lenasia Dynamos.

Shirikisho la soka la Zambia (FAZ)limetoa taarifa ya kuomboleza kifo cha Mulala likisema alikuwa sehemu ya kikosi cha Zambia cha mwaka 1984 kilichoshinda Kombe la East and Central Africa Challenge chini ya ukufunzi wake kanali Brightwell Banda.

Katibu Mkuu wa FAZ Adrian Kashala amesema chama cha soka kimepoteza mchezaji hodari.

Tunabaki na kumbukumbu nzuri ambazo marehemu Philemon alituheshimu nazo uwanjani. Kuna mengi ambayo wachezaji wa leo wanaweza kujifunza kutoka kwa kizazi cha marehemu,” Kashala alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!