October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mchezaji Bora Afrika kujulikana leo

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) leo linatarajia kutoa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2019, katika hafla inayotarajia kufanyika leo mjini Hurghada, Misri. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Riyad Mahrez anayecheza Manchester City, Sadio Mane na Mohamed Salah wote wanaocheza kwenye klabu ya Liverpool ya England.

Mahrez ambaye anatokea nchini Algeria amekuwa na msimu mzuri baada ya kuongoza timu yake ya taifa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika akiwa kama nahodha pamoja na kushinda ubingwa wa Ligi Kuu nchini England akiwa na klabu yake ya Manchester City.

Salah ambaye moja ya mchezaji anayepewa nafasi kubwa ya kushinda tena tuzo hii usiku huu kutokana na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya England, kuingoza klabu yake ya Liverpool kutwaa taji la ubingwa wa Ulaya.

Mchezaji mwengine aliyepewa nafasi ya kushinda tuzo hiyo usiku wa leo na wadau wengi wa soka ni mshambuliaji wa kutumainiwa wa timu ya taifa ya Senegal na Liverpool, Sadio Mane ambaye amekuwa na msimu mzuri 2019 baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa na kuisadia timu yake ya taifa kufika fainali ya AFCON.

Katika historia ya tuzo hizo wachezaji pekee walioshinda mara nyingi ni Yaya Tour aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast  na Samuer Eto’o ambao wote wameshinda mara nne.

 

 

 

error: Content is protected !!