Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Michezo Mchezaji aliyeishiwa nguvu baada ya kufunga, arejea kambini
Michezo

Mchezaji aliyeishiwa nguvu baada ya kufunga, arejea kambini

Crispin Ngush
Spread the love

 

CRISPIN Ngush, mchezaji wa Mbeya Kwanza nchini Tanzania, aliyefunga bao maridadi kisha kuishiwa nguvu na kupelekwa hospitalini, ameruhusiwa kurejea kambini kuungana na wenzake. Anaripoti Damas Ndembela,TUDARCo … (endelea).

Ngush alifunga bao hilo dakika ya 87 dhidi ya Mbeya City jana Jumapili, tarehe 3 Oktoba 2021, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22, Uwanja wa Sokoine jijini humo.

Lilikuwa ni bao la kushangaza la ‘bicycle-kick’ na kuinusuru timu yake kufungwa. Lilikuwa ni bao la kusawazisha na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa 2-2 na kuwafanya kugawana pointi.

Mara baada ya kufunga bao hilo, Ngush alikimbia akishangilia na kuruka sarakasi kisha alianguka china na kuchukuliwa na kupelekwa hospitalini.

Asubuhi leo Jumatatu, katika ukurasa wa kijamii wa Twitter wa Mbeya Kwanza iliyopanda daraja msimu huu, imeweka picha ya Ngush kuzungumzia hali ya mchezaji wake.

“Mpachika mabao wetu Crispin Ngush, aliyeishiwa nguvu baada ya kutufungua bao la kusawazisha na bao lake la pili jana na kukimbizwa Hospital, anaendelea vizuri na ameshajiunga na wenzake kambini lakini akiwa chini ya uangalizi wa Daktari. Tunashuru kwa sapoti yenu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!