August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mchengerwa ataka vilabu viwe na viwanja vyao

Spread the love

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amezitaka klabu nchini kuhakikisha wanamili viwanja vyao ili kukuza ustawi wa soka nchini, ambapo kwa sasa limeonekana kuwa na hamasa kubwa. Anaripoti Damas Ndelema …..(Endelea)

Mchengelwa ameyasema hayo jana tarehe 7 Julai 2022, katika hafla ya utoaji tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Johari Rotana.

Wakati akitoa hotuba yake kwa wageni waliodhuria hafla hiyo, Waziri huyo alisema kuwa, sera ya michezo nchini inazitaka klabu kuwa na viwanja vyao wenyewe kwani viwanja ambazo serikali itajenga na kukarabati ni kwa ajili ya mashindano makubwa

“Kuna vilabu vipo kabla hata nchi haijapata uhuru vinashidwaje kuwa na viwanja vyao naomba viongozi wa vilabu wawe wabunifu kama wanachama wapo tayari kuchangia changisheni “ Mchengerwa

Kwenye hafla hiyo Mchengerwa ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi, alifanikiwa kutao tuzo tatu, ikiwemo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyoenda kwa Yanick Bangala wa klabu ya Yanga.

Pia waziri ameziagiza Balaza la michezo Tanzania na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kumuandalia kikakao na watendaji wakuu wa vilabu ili wazungumze kwanini vilabu vinashidwa kuwa na viwanja vyao

Aidha waziri aliongelea mpango wa serikali ni kuandaa michuano ya AFCON 2027 kwani washatenga pesa ya ukarabati wa viwanja na viwanja hivyo vitakua vyenye ubora na viwango vya kuchezea mashindano ya kimataifa

error: Content is protected !!