October 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mchele, samaki vyapandisha mfumuko wa bei

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo

Spread the love

OFISI ya Taifa ya Takwimu, imesema mfumuko wa bei kwa kipimo cha Machi mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 4.3 kutoka asilimia 4.2 ya Februari kutokana na baadhi ya bidhaa kupanda bei. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo, amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Machi 2015,umeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa Februari.

Kwesigabo emesema, fahirisi za bei zimeongezeka hadi 155.88 kwa Machi 2015 kutoka 149.49 Machi 2014.

Amesema, mfumuko wa bei ya vyakula na viywaji baridi kwa Machi 2015, umeongezeka hadi asilimia 5.9 kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa Februari mwaka huu.

Kwesigabo ametaja baadhi ya bidhaa zinazochangia mfumuko wa bei na asilimia zake kwenye mabano kuwa ni mchele (19.9), samaki (14.5), choroko (13.1) unga wa muhogo (8.3), nyama (6.3), maharage (5.3) na sukari (4.4).

Kwa mujibu wa Kwesigabo, mfumuko wa bei wa Machi 2015, unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.7 ukilinganisha na ongezeko la asilimia 1.6 ya Februari mwaka huu.

“Uwezo wa Sh. 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh. 64 na senti 15 Machi 2015 kutoka Septemba 2010 ikilinganishwa na Sh.64 na senti 59 ya Februari mwaka huu.

“Kwa ujumla mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mfano mfumuko wa bei wa Machi 2015, umeongezeka kwa nchi tatu za Kenya, Uganda na Tanzania,” amesema Kwesigabo.

error: Content is protected !!