April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mchanganyo huu unaua virusi vya corona

Kondakta wa daladala akimnawisha mikono abiria kabla ya kuingia ndani ya gari

Spread the love

CHANGANYA lita moja ya Jik na lita sita za maji, kisha pulizia gari lao, hapo litakuwa salama dhidi ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Anyitike Mwakitalima, Mkuu wa Kitengo cha Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, ametoa kauli hiyo leo tarehe 14 Aprili 2020, wakati wa uhamasishaji kwa wananchi kuhusu tahadhari ya ugonjwa wa corona mkoani Mbeya na Songwe.

“Madereva na makondakta wote, kila siku jioni hakikisheni mnasafisha magari yenu kwa dawa maalum, wote mnaifahamu Jiki hapa, dawa hii inatumika kutakasa magari, bajaji au pikipiki.

“Changanya lita moja ya Jiki na lita sita (6) vya maji ili kupata mchanganyiko unaotakiwa kisha osha chombo chako cha kusafirisha abiria, utajikinga wewe na abiria wako,” amesema.

Amesema, kila dereva na kondakta wake ni lazima wahakikishe gari linakuwa na vitakasa mikono (Sanitizers), kwa ajili ya matumizi yao na abiria.

Pia, vituo vyote vya mabasi viwe na sehemu za kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kwani ni hatua muhimu sana ya kujikinga na virusi vya corona.

“Kondakta hakikisha kila anaepanda gari lako amenawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka au ametakasa mikono yake kwa Sanitizer ndio aruhusiwe kuingia kwenye gari, huu ugonjwa jamani ni hatari na umeua watu wengi,” amesema.

Aidha, amewaagiza madereva na makondakta wao kuhakikisha kila siku jioni wanapokuwa wamemaliza kazi zao wahakikishe wanasafisha magari yao kwa dawa maalum aina ya Jiki, ili kuua virusi vinavyoweza kuwepo na kupelekea maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Stafu Sajenti Valentino Ngowi, ofisa kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kamisheni ya Ushirikishaji Jamii, amewataka madereva bodaboda kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi endapo watakutana na mtu alieingia nchini kwa njia za panya.

“Sasa hivi kuna abiria wengi ambao wanaingia mkoani Mbeya kwa kupita njia za panya, na njia rahisi wanayotumia ni watu wa Bodaboda, hivyo tunawata msiingie kwenye vishawishi vya kutafuta hela ya haraka kwa kuwapitisha watu hao, jambo ambalo ni kinyume na sheria,” amesema.

Mbali na hayo, Ngowi amewataka madereva wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanafuata sheria bila shuruti, ikiwemo kuhakikisha abiria hawasimami kwenye magari (level seat), na Bajaj wapande abiria watatu tu.

error: Content is protected !!