
John Magufuli, Rais wa Tanzania (kushoto) akiwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo
RAIS Rais John Magufuli ameanza kutekeleza ushauri aliopewa katika ripoti ya Kamati ya kuchunguza makontena ya mchanga wa madini yaliyokamatwa kwa kumtengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, anaandika Hamisi Mguta.
Wakati Rais Magufuli anapokea ripoti hiyo Ikulu alimtaka Profesa Muhongo ajitathmini kuhusu nafasi yake ya uwaziri baada ya kupokea ripoti ya mchanga wa madini Ikulu kutokana na kushindwa kusimamia vyombo vilivyochini yake.
Hata hivyo, kabla ya Profesa Muhongo kutoa kauli yoyote Rais ametengua uteuzi wake kuanzia leo. Nafasi ya Profesa Muhongo itajazwa baadae.
More Stories
Dk. Mwigulu, Bashungwa wawekwa kikaangoni
Samia azindua mradi wa maji wa Sh. bilioni 2.8
Samia kuhusu bei ya mafuta: Ni tatizo la dunia nzima