NI kama mchakato wa kumtafuta kocha mpya wa klabu ya Simba umeendelea kupamba moto, kufuatia mpaka sasa uongozi wa klabu hiyo kupokea wasifu wa makocha zaidi ya 100, huku kocha wa sasa wa APR ya Rwanda Erradi Mohammed Adil raia wa Morocco, akipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)
Simba imejikuta kwenye mchakato huo, mara baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wao Pablo Franco Martini raiaa Hispania, ambaye alitimuliwa na uongozi wa klabu hiyo kufuatia matokeo mabovu waliyoyapata Simba katika msimu huu.
Kocha huyo raia wa Morocco anapewa nafasi kubwa, kutokana na viongozi wa klabu ya Simba kumtaka kocha ambaye analijua vizuri soka la barani Afrika, na hivyo mmoja ya vigezo vyao ni kuchagua kocha ambaye anatoka ndani ya bara la Afrika.
Vigezo hivyo vinathibitisha na manane aliyonukuliwa mtendaji wa klabu ya Simba katika siku za hivi karibuni kupitia Simba App, na kusema kuwa, kwa sasa wanahitaji kocha mzawa wa bara la Afrika.
“Tunahitaji Kocha anayejua vizuri soka la Afrika pia tungefurahi kupata Kocha ambaye ni mzawa wa bara hili lakini mpaka sasa bado hawajatuma wasifu na aliteyuma mmoja na vigezo vyake havitoshi” alisema Barbara
Akizungumzia idadi ya wasifu waliopokea mpaka sasa, mtendaji huyo alisema kuwa wapokea wasimu wa makocha zaidi ya 100 huku wengi wao wakitokea barani Ulaya, lakini mchakato huo huwenda ukakamilika wiki mbili zijazo.
“Tumepokea wasifu wa makocha zaidi ya 100 kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao wengi wao ni kutoka barani Ulaya na Amerika Kusini. Mchakato wa mchujo unaendelea na tunategemea utakamilika ndani ya wiki mbili zijazo” Alisema Barbara
Kuelekea msimu ujao, klabu hiyo imedhamilia kufanya mabaliko makubwa kwenye benchi lao la ufundi, kufuatia kumaliza msimu huuu bila taji lolote.
Simba iliamua kumtimua Pablo siku chache mara baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam, dhidi ya Yanga ambao ulipigwa kwenye dimba la CCM kirumba, Mwanza.
Makubaliano ya Simba kumvunjia kocha huyo mktaba, yalifikiwa Mei 31 mwaka huu, na klabu hiyo ilimtakiwa kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya klabu hiyo.
Pablo alijiunga na Simba tarehe 10 Novemba 2022, Akichukua nafasi ya Didier Gomes, ambaye aliamua kuachana na timu hiyo kufutai matokeo mabaya aliyoyapata kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwenye msimu huu.
Toka alipofika nchini Pablo amefanikiwa kuwapa Simba taji moja tu, la michuano ya kombe la Mapinduzi mara baada ya kuwafunga Azam FC kwenye fainali.
Leave a comment