Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mchakato uvunjaji Jiji la Dar wahojiwa bungeni
Habari za Siasa

Mchakato uvunjaji Jiji la Dar wahojiwa bungeni

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam
Spread the love

 

SERIKALI imeombwa kupitia upya mchakato wa ugawaji mali za iliyokuwa Jiji la Dar es Salaam, baada ya kuvunjwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Alhamisi, tarehe 24 Juni 2021 na Mbunge wa Mbagala mkoani Dar es Salaam(CCM), Abdallah Chaurembo, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo wa Mbagala amedai kuwa, mchakato wa ugawaji mali hizo haukuwashirikisha wabunge na mabaraza ya madiwani ya mkoa huo, hali iliyopelekea mgawo wake kutokuwa sawa.

“Kwa kuwa mgawanyo wa mali wa iliyokuwa Jiji la Dar es Salaam, haukushirikisha wadau wakiwepo wabunge na mabaraza ya madiwani. Je, Serikali haioni iko haja ya kui-review (kupitia) ule mgawo, hasa katika mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu?” Amehoji Chaurembo.

Abdallah Chaurembo, Mbunge wa Mbagala (CCM)

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, David Silinde, amesema Serikali italifanyia kazi ombi hilo, ili kubaini kama mchakato huo haukushirikisha wadau, kwa ajili ya kuangalia namna ya kuwashirikisha.

“Jambo alilolileta mbunge ni kubwa, inahitaji tufuatilie na tujiridhishe. Kwa sababu nina imani kila jambo linapofanyika kunakuwa na muhutasari, ambao huwa unaandikwa na vikao na idadi ya watu waliohudhuria,” amesema Silinde na kuongeza:

“Endapo jambo hili halikufanyika, basi ninaamini Tamisemi itazingatia namna bora kabisa, itakayosaidia jambo hili kufanyika kwa ukamilifu. Tutalipokea na kufanyia marekebisho.”

Jiji la Dar es Salaam lilivunjwa na Magufuli tarehe 24 Februari mwaka huu, ambapo aliipandisha hadhi iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, kuwa Jiji la Dar es Salaam.

Magufuli aliyefariki dunia akiwa madarakani tarehe 17 Machi 2021, alilivunja jiji hilo kwa maelezo kwamba, waliokuwa viongozi wake hawakuwa na eneo wanalowawakilisha wananchi, licha ya kutengenewa bajeti na posho, kitendo kilichosababisha matumizi mabaya ya fedha za umma.

Katika hatua hiyo, waliokuwa watumishi wa jiji hilo, walihamishiwa katika vituo vingine vya kazi, huku mgawanyo wa mali na madeni ya yaliyokuwa ya jiji hilo, ulifanyika kwa mujibu wa sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

error: Content is protected !!