January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mch. Mtikila apumzishwa

Spread the love

MWILI wa aliyekuwa muasisi na mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila, umepumzishwa kijijini kwake, Ludewa mkoani Iringa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mtikila alifariki dunia Jumapili iliyopita baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali katika eneo la Msolwa, Chalinze, mkoani Pwani.

Misa ya kumuaga mwanasiasa huyo machachari nchini, ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri, Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumza kabla ya shughuli ya kuaga mwili wa Mchungaji Mtikila kuanza, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, aliwaeleza waombelezaji kuwa Mchungaji Mtikila alikuwa mmoja wa wanasiasa imara na kuwataka viongozi wengine wa kisiasa kuiga mfano wake.

“Mchungaji Mtikila alikuwa mtu wa kusimamia na kufuatilia kile anachokiamini. Alikuwa akifanya harakati zake kwa kufuata sheria,” alieleza Jaji Mtungi

Mtikila alijizolea umaarufu mkubwa nchini baada ya kuonesha dhamira yake ya dhati ya kupigania taifa lake la Tanganyika kutaka lilirejeshwe.

Hata hivyo, katika miaka ya mwisho ya uhai wake, Mchungaji Mtikila amekuwa akitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Usalama wa Taifa (TISS), kudhoofisha juhudi za ukombozi, kwa kushambulia na kuwazushia baadhi ya viongozi wandamizi wa upinzani na wanaharakati wengine.

error: Content is protected !!