October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mch. Msigwa apigwa ‘stop’ kufanya mikutano Iringa

Mch. Peter Msigwa

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Iringa limempiga marufuku Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa kufanya mikutano ya hadhara kwa madai ya kutoa lugha za matusi na uchochezi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa barua iliyosambaa mitandaoni inayodaiwa kutoka kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Iringa na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wilayani humo, Yohana Mjengi, inadai kuwa Msigwa amekiuka makubaliano ya kibali alichopewa cha kufanya mikutano hiyo.

Barua hiyo inaeleza kuwa, Katika barua yake ya maombi, Msigwa aliomba kufanya mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali, kwa ajili ya kukutana na wananchi, kupokea kero, kuhamasisha maendeleo na kupokea maoni kabla kwenda bungeni.

Lakini, barua hiyo inadai kuwa, Msigwa katika mkutano wake wa hadhara alioufanya kwenye kata ya Kihesa, alitoa maneno ya kashfa na uchochezi yanayoashiria uvunjifu wa amani kwenye jimbo lake na kwamba kwa mantiki hiyo haruhusiwi kuendelea na mikutano yake, hivyo kama akikaidi agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa mara moja dhidi yake.

received_155963048681709

error: Content is protected !!