Sunday , 25 February 2024
KimataifaTangulizi

McCain afariki dunia

Spread the love

MPINZANI was Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama mwaka 2008 na seneta maarufu nchini Marekani, John McCain (81), amefariki dunia akiwa katika chumba chake cha mapumziko. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

McCain alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya ubongo, amefariki katika chumba chake cha mapumziko mjini Sedona, Arizona, akiwa na familia yake.

Aidha, mwanasiasa huyo mkongwe aligundulika kuwa na ugonjwa huo hatari mwezi Julai mwaka 2017 ndipo alipoanza matibabu rasmi.

McCain aliwahi kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican mara mbili, na kuteuliwa kama mgombea rasmi mwaka wa 2008 ambapo alipambana na kushindwa na mgombea wa chama cha Demokratic, Barack Obama.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa maombi yake anayaelekeza kwa familia ya Seneta McCain ambaye aliwahi kulitumikia bunge la Marekani kwa miongo mitatu.

Pia aliwahi kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican mara mbili, na kuteuliwa kama mgombea rasmi mwaka wa 2008 ambapo alipambana na kushindwa na mgombea wa chama cha Demokratic, Barack Obama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

error: Content is protected !!