Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Michezo Mbwana Samatta ajiunga Fenerbahce ya Uturuki
Michezo

Mbwana Samatta ajiunga Fenerbahce ya Uturuki

Spread the love

NAHODHA wa timu ya soka la Tanzania ‘Taifa stars’ Mbwana Samatta amejiunga na Fenerbahce ya Uturuki kwa mkataba wa miaka minne kutoka Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Leo Ijumaa asubuhi tarehe 25 Septemba 2020, Mtandao wa Fenerbahce inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki umeweka picha za Samatta akisaini mkataba na timu hiyo.

Samatta alijiunga na Aston Villa akitokea KRC Genk ya nchini Ubelgiji katika dirisha dogo la usajili Januari 2020 kwa mkataba wa miaka minne na nusu.

Nahodha huyo wa Taifa Stars amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya Uingereza.

Akiwa Aston Villa inayofundishwa na Kocha Dean Smith, Samatta alicheza michezo 16 ya mashindano na kufunga magoli mawili pekee.

“Najua Fenerbahce ni timu kubwa siyo tu hapa Uturuki, ni klabu yenye uzito wake duniani,” amesema Samatta aliyezaliwa tarehe 23 Desemba 1992 jijini Dar es Salaam.

Samatta amesema “nina furaha kuwa katika familia hii kwa sababu itakuwa changamoto mpya na kubwa kwangu. Fenerbahce ina mashabiki wengi na wakati wote wanahitaji ushindi na tunahitaji kushinda. Nimekuja na ninafuraha na matumaini tutashinda mataji mengi.”

1 Comment

  • Моё почтение, моя любимая газета. Я приобретаю колосасальное блаженство от прочтения Именно ваших публикаций!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

Michezo

Meridianbet inakwambia beti mechi spesho za EURO sasa

Spread the love Wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wamekuja na Spesho ODDS...

error: Content is protected !!