WILBROAD Qambalo, Mbunge wa Jimbo la Karatu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anasakwa na Jeshi la Polisi Karatu, anaandika Faki Sosi.
Kwa mujibu wa barua ya wito ya jeshi hilo, Qambalo na viongozi wengine wa chama hicho wilayani humo wanasakwa na polisi ili kuhojiwa kwa madai ya kufanya mkutano wa hadhara.
Kwa mujibu wa barua hiyo, viongozi hao walifanya mkutano wa hadhara tarehe 23 Julai mwaka huu katika eneo la Tloma lililopo Kata ya Ganako, Karatu Mjini.
Wengine wanaotafutwa ni pamoja na Cecilia Pareso, Mbunge Viti Maalum na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo .
Kwa mujibu wa barua hiyo iliyotoka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Jinai, Wilaya ya Karatu iliyoandikwa leo, imemtaka Qambalo kufika kwa Mkuu wa Upelelelezi Mkoa wa Arusha leo.
More Stories
Lissu, Prof. Assad wapenyeza ‘sms’ Ikulu
Rais Kenyatta atuma ujumbe Tanzania, Samia atoa maagizo
CCM wataka NDC ing’olewe miradi Mchuchuma, Liganga