August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge wa CUF aburuzwa mahakamani

Abdallah Mtolea, Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF)

Spread the love

ABDALLAH  Mtolea, Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), amefikishwa  mahakamani kwa kosa la usalama barabarani, anaandika Hamisi Mguta.

Kamanda mkoa wa Polisi Temeke, Gilles Mroto,  akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu amesema, Mtolea alikamatwa jana na amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa makosa ya kuendesha gari lisilokatiwa bima na kushindwa kutii amri ya askari wa usalama barabarani.

Mtolea alikamatwa jana majira ya saa moja usiku na alikuwa akikabiliwa na makosa ya kuendesha gari bila ya bima kwa muda wake ulimalizika tangu Desemba 26  mwaka jana.

Kwa mujibu wa maelezo ya kamanda Mroto, Mtolea alikaidi agizo la askari wa usalama barabarani la kumtaka asimame badala yake alikaidi na kuwasha gari na kuondoka.

error: Content is protected !!