Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge wa Chadema apata ajali mbaya
Habari za Siasa

Mbunge wa Chadema apata ajali mbaya

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kunti Yusuf Majala, amejeruhiwa vibaya baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali. Anaripoti Yusuph Katimba … (endelea).

Ajali hiyo ilitokea leo Jumatatu, tarehe 24 Desemba, maeneo ya Kilema, katikati ya wilaya za Chemba na Kondoa.

Taarifa zilizothibitishwa na ofisa mmoja wa Bunge mjini Dodoma, ambaye hata hivyo, hakupenda kutajwa jina lake, zinaeleza kuwa katika ajali hiyo, watu wengine wawili wamefariki dunia.

Afisa huyo ambaye anasema siyo msemaji wa Buge, anaeleza kuwa gari ambalo mbunge alikuwa akilitumia lilianguka baada ya kuchomoka tairi la mbele mkono wa kushoto wa dereva.

Anasema, “gari hili lilikuwa na watu 11 (kumi na moja), watoto saba na wakubwa wanne. Mhe. Kunti ana maumivu makali sana ya kiuno na shingo.”

Anasema, kufuatia hali ya mbunge huyo kuwa mbaya, ofisi ya Spika, imeanza kufanya utaratibu wa haraka wa kuhakikisha mara atakapofikishwa kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, aweze kusafirishwa yeye na majeruhi wengine, kupelekwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.”

Hata hivyo, afisa huyo hakuweza kuwafahamu mara moja majina ya wale waliofariki dunia; na au kujeruhiwa. Bali, taarifa kutoka maofisa wa Chadema zinasema, baadhi yao waliofariki, sehemu kubwa watakuwa familia ya mbunge huyo.

Kwa mashuhuda, gari lililokuwa limembeba Kunti na ambalo limepata ajali, lilikuwa na namba za usajili, T 624 DPE. Lilikuwa likitokea Dodoma mjini kuelekea Kondoa.

Dereva wa gari hilo alikuwa ni Stephano Masawe, ambaye ni dereva wa Katibu wa Chadema, Kanda ya Kati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!