January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge wa CCM agawa “rushwa” usiku

Mbunge wa Kwimba, Mhe. Mansoor Shanif Hiran (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Spread the love

WAKATI wabunge wakihaha kutetea majimbo yao katika uchaguzi mkuu mwaka huu, Mbunge wa Kwimba mkoani Mwanza, Shanif Mansoor (CCM), anadaiwa kugawa fedha wa wafuasi wake usiku wa manane katika nyumba ya kulala wageni. Anaandika Mwandishi wetu … (endelea).

MwanaHALISIOnline limedokeza kuwa, Mansoor anakabiliwa na wakati mgumu jimboni kwake, kutokana na kulalamikiwa na wapiga kura kuwa, haonekani tangu achaguliwe, jambo linalotajwa kama sababu ya kulazimika kutumia fedha kuweka mambo sawa.

Hata hivyo, alipotafutwa kujibu madai hayo, Mansoor alikiri kuwepo kwa kikao baina yake na wanachama wa CCM, akisema kilifanyika kati ya saa nne hadi saba  usiku.

“Kwani kuna kosa gani mimi nikiwapa wajumbe posho? Alihoji alipoulizwa kuhusu madai ya kugawa rushwa na kuongeza kuwa, “nafahamu hayo yote yanotokana na siasa na huu uchaguzi mkuu ujao.”

Licha ya Mansoor kukana kugawa rushwa kwa wajumbe akidai ni posho, chanzo chetu kinasema kuwa mbunge huyo amekuwa na desturi ya kutumia fedha kuwalainisha wananchi baada ya kubaini hali yake ni tete kisiasa.

Hata kikao cha siri anachodaiwa kukiitisha mbunge huyo usiku katika ukumbi wa nyumba ya kulala wageni (jina linahifadhiwa), kimewagawa wanachama wenzake wa Chama Cha Mapinduzi, wakidai sio utaratibu.

“Kama kikao hicho kingekuwa ni cha kujenga chama, wasingefanya kwa siri hivi tena usiku. Wanachama waliohudhuria wametoka huko wakilalamika kupotezewa muda na wakapewa Sh. 5000,” amesema kada mmoja wa CCM.

Katika uchaguzi mkuu uliyopita mwaka 2005, Mansoor alichuana vikali na Leticia Nyerere (Chadema). Na sasa kutokana na Chadema kujiimarisha zaidi ikiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), CCM ina wakati mgumu wa kulitetea jimbo hilo.

error: Content is protected !!