Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge: Serikali inawawekea vikwazo wananchi Ngorongoro
Habari za Siasa

Mbunge: Serikali inawawekea vikwazo wananchi Ngorongoro

Spread the love

MBUNGE wa Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai ameituhumu Serikali “inawawekea vikwazo vya kimaendeleo” wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa kuhamisha fedha za miradi kwenda Handeni mkoani Tanga. Anaripoti Gabriel Mushi…(endelea).

Ole Shangai ameyasema hayo Bungeni leo Jumatato tarehe 13 Aprili 2022, wakatyi akichangia hoja ya hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zake ya mwaka 2022/23.

Licha ya kumshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kukubali kusikiliza maoni ya wananchi na kuwataka kuhama kwa hiari Ole Shangai alidai kuna tatizo la wanaobaki kuwekewa vikwazo.

“Kuna tatizo moja, wale wanaobaki inaonekana Serikali wanawawekea vikwazo vya kimaendeleo, kuna fedha ambazo zilipelekwa kwaajili ya vituo vya afya, kwaajili ya maji, kwaajili ya madarasa inaonekana sasa Serikali inaamisha zile fedha kwenda Halmashauri ya Handeni. Walimu wameandikiwa, vituo vya afya vimeandikiwa hizo fedha ziende Handeni.

“Ninachojiuliza sasa Serikali imeona wa muhimu ni wale walio na hiari ya kuondoka na wale watakaobaki itakuwaje. Kama tunawanyima vituo vya afya, maji, shule je wale wananchi watakuwa sehemu ya Watanzania?” alihoji.

Baada ya kuibua tuhuma hizo Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa aliomba kumpa taarifa na kueleza bungeni hapo kuwa Serikali inapeleka miradi Handeni na Ngorongoro pia.

“Wananchi wote ni wakwetu kule Handeni tunapeleka maendelo lakini pia Ngorongoro miradi inaendelea, asubiri bajeti yangu aone namna tulivyojipanga kuahakikisha hata tarafa ya Ngorongoro inaenda kama kawaida,” amesema Bashungwa.

Hata hivyo Ole Shangai alikataa kupokea taarifa hiyo kwa kuhoji sababu ya wananchi wa tarafa hiyo kusubirishwa bajeti ijayo huku fedha walizokuwa wamepewa zikihamishwa kutoka kenye akaunti kwenda Handeni.

“Fedha Sh 500 milioni za kituo cha afya Nainokanoka zimehamishwa kupelekwa Handeni, Sh 600 milioni za maji kata za Ailelai, Masamburai, Olbalbai na maeneo mengine mnahamisha kwaajili ya kuwawekea wananchi vikwazo vya maendeleo,” amesema Ole Shangai.

Waziri wa Maji Juma Aweso naye aliomba kumpa taarifa Mbunge huyo na kueleza kuwa hakuna maelekezo yeyote ya Serikali kwamba wananchi wa Ngorongoro wasipelekewe maji.

“Katika jimbo la Ngorongoro tumepelaka mitambo ya kuchimba maji na Waziri Mkuu alielekeza wananchi wapate huduma ya maji katika jimbo hilo,” amesema Aweso.

Licha ya kuipokea taarifa hiyo Ole Sangai alidai kuwa maji hayo hayachimbwi tarafa ya Ngorongoro bali ni katika tarafa zingine za Loliondo na Sale.

Ameongeza kuwa hata Hospitali ya Enduleni iliyokuwa inapata Sh 500 milioni kutoka Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwaajili yakuwatibu watu, fedha hiyo imeondolewa pia.

“Kwahiyo watoto wa dogo, kina mama wanakufa kwa kukosa huduma, hasa serikali gani hii ambayo inawawekea vikwazo wananchi.

“Kama tunataka kupunguza wananchi Ngorongoro sio kwa namna hiyo ya kuwawekea vikwazo vya kimaendeleo.

Naibu Waziri wa Afya Godwini Mollel naye alimpa taarifa kuwa Sh 321 milioni za Global Fund zimetengwa kuelekea eneo la Enduleni, “naomba mheshimiwa mbunge usiwe na hofu.”

Lichaya taarifa ya Naibu Waziri, mbunge huyo aliendelea kulalama kuwa vituo havina dawa na kwamba hata wananchihivi sasa wanakaguliwa kuingia getini na wanarudishwa.

Amesema suala lingine ni zoezi linaloendelea la Anwani ya makazi, “kule Ngorongo hakuna zoezi hilo katika tarafa ya Ngorongoro.”

Naye Naibu Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Methew amempa taarifa kuwa Serikali inajenga minara 24 katika Jimbo la Ngorongoro na zoezi la anwani za makazi linaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!