October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge: Polisi Liwale hawana jengo kwa miaka 47

Zubeir Kuchauka

Spread the love

MBUNGE wa Liwale, Zubeir Kuchauka (CCM), amesema Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, haina jengo la Kituo cha Polisi kwa muda miaka 47, badala yake limepanga katika jengo la benki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo Alhamisi, tarehe 22 Septemba 2022, Kuchauka alihoji kauli ya Serikali kuhusu wilaya hiyo kupatiwa jengo la Kituo cha Polisi.

“Wilaya ya Liwale ina umri wa miaka 47, sasa haijawahi kuwa na jengo la kituo cha polisi, ukiacha lile jengo ambalo wamepanga lilikuwa la benki. Nini kauli ya Serikali kuipatia Wilaya ya Liwale jengo la polisi,” amesema Kuchauka.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.

“Tunafahamu wilaya kongwe hizi zimekuwa na vituo lakini chakavu sana, sasa kwa bahati mbaya Liwale hawajawahi kuwa nacho. Nimuahidi katika bajeti ijayo tutaweka kipaumbele ili wilaya yako ianze mchakato.

error: Content is protected !!