August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge: Odinga ni kigeugeu

Raila Odinga, Kiongozi wa ODM (kushoto) akiwa na Mbunge wa Ruiru, Issac Mwaura

Spread the love

ISAAC Mwaura, Mbunge wa kaunti ya Ruiru, Wilaya ya Kiambu nchini Kenya amesema, Raila Odinga ni kigeugeu, anaandika Wolfram Mwalongo.

Taarifa iliyoripotiwa na mtandao wa Nairobi News zinaeleza kuwa, Mwaura kutoka katika Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kinachoongozwa na Odinga ametoa kauli hiyo siku moja baada ya yeye (Mwaura) na wenzake tisa kutajwa kuwa miongoni mwa wanachama watakaofukuzwa kwa madai ya kuhujumu chama hicho.

Mwaura aliyewahi kuwa mshauri mkuu wa Odinga alipokuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo amesema sasa ameelewa maana ya neno kigeugeu, ambalo limekuwa likitumiwa na watu wengi ndani na nje ya taifa hilo.

“Na huyu Raila kweli sio muungwana, nilimuheshimu, ilikuwa nikienda kwake kuongea mengi kuhusu uhalisia wa siasa,.. sasa nimefahamu kwanini watu wanatumia neno kigeugeu..,” amesema Mwaura.

Hata hivyo, miongoni mwa majina yaliyotajwa kupitiwa na fagio hilo ndani ya chama hicho ni pamoja na Salim Mvurya, Gavana wa Kwale; Adabu Namwamba, Mbunge wa Budalang’i; JohnWaluke, Steven Kairukin na Zainab Chidzuga (mwakilishi wa wanawake).

Mbunge huyo ambaye ndio wa kwanza mwenye ulemavu wa ngozi (albino) kuingia katika bunge la nchi hiyo amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha chama chake kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya jamii.

Awali kupitia ukurasa wake wa Facebook alindika kwamba, Uhuru Kenyatta, Rais wa taifa hilo amekuwa tayari kushirikiana na wapinzani ingawa uongozi wa chama chao umekuwa ukijivuta kuunga mkono jitihada hizo.

“Mheshimiwa Rais Kenyatta amedhamiria ushirikishwaji wa makundi kihistoria wasiojiweza katika agenda na rasilimali za kitaifa mgao. Ilikuwa ajenda yangu,” amesema Mwaura.

error: Content is protected !!