May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Nyongo ahoji barabara Maswa-Lalago, serikali yamjibu

Mbunge wa Maswa Mashariki (CCM), Stanslaus Nyongo

Spread the love

 

MBUNGE wa Maswa Mashariki (CCM), Stanslaus Nyongo, amehoji lini serikali itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwamgo cha lami ya Maswa hadi Lalago. Anaripoti Jemima Samwel, DMC …(endelea).

Amesema hayo leo Jumatano, tarehe 19 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na maiibu bungrni jijini Dodoma.

Mbunge huyo amesema, barabara hiyo ni ya muda mrefu imekaa bila kuweka lami jambo ambalo si sawa.

“Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Maswa hadi Lalago?”

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Msongwe Kasekenya amesema, barabara ya Maswa – Lalago yenye urefu wa kilometa 34 ni barabara ya mkoa inayohudumiwa na wizara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (Tanrods).

“Barabara hii ni sehemu ya mradi wa Serengeti Southern bypass ikianzia Maswa – Lalago -Mwanhuzi – Sibiti hadi Karatu yenye urefu wa kilometa 338.”

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Msongwe Kasekenya

“Mradi huu ulihusisha kazi ya peumbuzi yakinifu chini ya ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na umeshakamilika. Kwa sasa, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza usanifu wa kina na ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami,” amesema Kasekenya

“Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali sehemu hii ya Maswa – Lalago na inapitika majira yote ya mwaka,” amesema Kasekenya

Akiuliza maswali ya nyongeza, Nyongo aliyewahi kuwa naibu waziri wa madini ameuliza “ni lini hasa ujenzi utaanza.”

Akijibu swali hilo, Mhandisi Kasekenya amesema, mara baada ya kupata fedha ujenzi huo utaanza.

error: Content is protected !!