March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge mwingine Chadema aachia ngazi

Spread the love

ALIYEKUWA mbunge wa Simanjiro (CHADEMA), James Millya, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika barua yake kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Millya anasema, ameamua kuchukua uamuzi huo kufuatia kuona giza nene kwa chama alichokuwa.

Anasema, kabla ya kujiunga na Chadema alikuwa mwanachama wa CCM. Anasema, aliondoka CCM kwa kuwa alikiona siyo chama chenye kutetea maslahi ya wengi.

“Nilikuwa Chadema, lakini sasa nimeona kuwa haina mpango wa kutetea kile ninachokiamini,” ameeleza Millya.

IMG-20181007-WA0043

error: Content is protected !!