July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Manyoni atangaza neema jimboni

Spread the love

MBUNGE mteule wa jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka (CCM) amewatangazia neema wananchi wa jimbo hilo na kuwaahidi kwamba kipaimbele cha kwanza katika jimbo hilo ni kutatua migogoro ya ardhi. Anaandika Dany Tibason, Manyoni … (endelea).

Mtuka ambaye awali alikuwa Kamanda wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) kanda maalum ya Dar es Salaam amesema Manyoni ni kati ya wilaya ambayo inakabiliana na changamoto nyingi ambazo zinatakiwa kutatuliwa.

Alitoa kuali hiyo muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika jimbo hilo ambalo awali lilikuwa likiongozwa na mkongwe wa siasa Kapteni Mstaafu John Chiligati.

Mtuka amesema Manyoni kuna changamoto nyingi ambazo wananchi wanakabiliana nazo ikiwa ni pamoja na uhaba wa maji, migogoro ya ardhi huku akisema ni pamoja na kutafuta mbinu za kuwawezesha vijana kuondokana na umasikini.

Mteule huyo ambaye alithubutu kugombea nafasi hiyo mwaka 2010 na kushindwa katika kura za maoni kwa sasa amefanikiwa baada ya kushinda kura za maoni katika chama hicho na hatimaye kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu.

Akizungumza na wananchi wa Manyoni Mtuka amesema katika jimbo hilo kuna fursa nyingi ambazo vijana wataweza kujihusisha nazo ili kuondokana na maisha ya kukaa vijiweni.

Jambo lingine ambalo Mtuka amesema atashughulika nalo ni kuhakikisha wazee wanapata huduma bora ya afya na bure kama sera inavyojieleza.

Akizungumzia elimu amesema ni wajibu wa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule kuwa shuleni na si vinginevyo.

error: Content is protected !!