January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Mafia alalamikia serikali

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalumu Jimbo la Mafia, Riziki Ngwali amelalamika kwamba serikali imeisusa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia katika huduma za afya. Anaandika Faki Sosi … (endelea)

Akizungumza na MwanaHALISI Online mbunge huyo amesema kuwa, hospitali ya wilaya hiyo haina dawa wala vifaa tiba na kusababisha akazi wa Mafia kutaabika.

Ngwali amesema kuwa, amesikitishwa na kauli ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa iliyotaka halmashauri zijitegemee wakati hazina pesa ya kutosha jambo linalosababisha huduma muhimu kwenye halmashauri mbalimbali nchini kushindikana.

Amesema kuwa, hospitali hiyo imekuwa ikilalamikiwa mara kwa mara na wananchi kwa kukosa huduma stahiki zaidi ya kuandikiwa dawa na vifaa tiba vinavyouzwa kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi.

“Hata mimi mwenyewe niliwahi kumpeleka kijana wangu hospitalini hapo, hapakuwa na dawa ya aina yoyote wala vifaa tiba ambapo tulikosa hata bomba la sindano,” amesema Ngwali.

Amesema kwa ujumla wilaya hiyo haina huduma bora za afya kutokana na kuwa na uhaba wa wataalamu kwenye wilaya hiyo ambapo imepelekea wahudumu wa afya kufanya shughuli za utatibu.

Gazeti la MwanaHALISI toleo namba 320 la Januari 4, 2016 lilipokea barua ya malalamiko kutoka kwa mmoja wa wasoji wa gazeti hilo ambaye ni makazi wa Wilaya ya Mafia aliyekuwa akilalamikia hospitali hiyo ambapo alieleza kuwa kwenye hospitali hiyo hakuna dawa wala vifaa tiba ambapo imepelekea mtu akipata tatizo lazima asafirishwe Jijini Dar es Salaam.

Kwa wakati mwengine Ngwali amesema kuwa, changamoto nyengine ni ubinafsi wa mbunge wa Chama Cha Mapindu (CCM) kutokana na kutoshiriki kwenye vikao muhimu vya maendelea ya halmashauri.

error: Content is protected !!