Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge kutumia milioni 480 kujenga ofisi za CCM
Habari za Siasa

Mbunge kutumia milioni 480 kujenga ofisi za CCM

Spread the love

 

MBUNGE wa Igunga mkoani Tabora, Nicholas Ngassa (CCM), anatarajia kutumia kiasi cha Sh milioni 480 kwa ajili ujenzi wa ofisi za kata za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye kata 16 za jimbo hilo. Anaripoti Victor Makinda, Tabora … (endelea).

Ngassa ametoa kauli hiyo jana tarehe 22 Januari, 2023 wilayani Igunga wakati akizungumza katika hafla ya kukabidhi ramani ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT).

Pia alikabidhi matofali 1000 na mifuko ya sementi 100.

Alisema moja ya ahadi aliyoitoa kwa wanachama wa CCM Igunga wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ni kujenga ofisi za chama kwenye kata zote 16 kupitia fedha zake binafsi.

Alisema mpango huo wa ujenzi wa ofisi hizo upo tayari na unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni huku matarajio yakiwa ni kukamilisha ujenzi huo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

“CCM ni chama kikongwe na ni chama kikubwa kinachoaminiwa, kupendwa na kutegemewa na mamilioni ya Watanzania. Ni lazima kiwe na miundombinu wezeshi itakayowarahisishia watendaji wake kufanya kazi kwa ufanisi,” alisema Ngassa.

Ngasa alisema kwa kutambua umuhimu wa chama hicho kuendelea kujijenga kuanzia ngazi za chini na kwa mapenzi makubwa aliyonayo kwa chama chake, ameamua kutumia fedha zake binafsi zinazotokana na mshahara wake na vyanzo vyake vingine vya mapato kuhakikisha kuwa kata zote zinakuwa na ofisi ambazo zitakuwa na sehemu ya ukumbi wa mikutano na vyumba vitatu vya biashara.

“Lengo sio kuwa tu na ofisi, bali ni kuwa na chanzo cha mapato cha uhakika kwa jumuiya za chama. Ofisi za kata ninazotarajia kuanza ujenzi wake hivi karibuni.

“Pia zitakuwa na vyumba vitatu vya biashara vitakavyotumika kwa shughuli za ujasiriamali ili pato litokanalo liweze kusaidia ustawi wa jumuiya za chama ikiwa ni Jumuiya ya Vijana (UVCCM) Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa wanawake (UWT),” alisema.

Aidha, alisema anatarajia kuwanunulia baiskeli makatibu wa matawi yote, pikikpiki kwa makatibu kata wote wa chama hicho jimboni Igunga.

“Kazi ya makatibu wa Kata na matawi ni kubwa, natambua kuwa usafiri ni kikwazo kwao kuwafikia wanachama kwa haraka, moja ya mipango yangu ni kuwanunulia baiskeli na pikipiki ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi kuendana na kasi ya siasa za wakati huu,” alisema.

Katibu wa CCM wa kata ya Mwamakona, Robert Madutu alisema ujenzi wa ofisi hizo na vyombo vya usafiri wanavyotarajiwa kupewa na mbunge wao utawaongezea ufanisi wa kazi ya uenezi wa chama hicho.

Akizungumza kuhusu utekelezaji wa ahadi ya Mbunge huyo kwa ustawi wa chama, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Igunga, Mafunda Temanywa alisema CCM wilaya hiyo imefarijika kuona kuwa kuna mwanachama mwenye moyo wa kujitolea katika kukijenga na kukiimarisha.

“Ninaamini kilichomsukuma mbunge wetu kujenga ofisi za chama ni uzalendo wake, dhamira yake na mapenzi yake mema kwa chama CCM, hivyo ninatoa wito kwa wanachama wengine kuwa tayari kujitoa kwa hali na mali katika kukijenga CCM,” allsema Mafunda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!