Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Ilemela atishwa
Habari za Siasa

Mbunge Ilemela atishwa

Angelina Mabula, Mbunge wa Jimbo la Ilemela
Spread the love

ANGELINA Mabula, Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mwanza amemtishwa na wapiga kura wake kwa madai ya kushindwa kutatua kero ya mgogoro wa ardhi, anaandika Moses Mseti.

Wananchi wapatao 7500 katika Mtaa wa Jiwe Kuu, Kata ya Kitangiri iliyopo wilayani Ilemela wamemlalamikia Mabula kwa kushindwa kutatua mgogoro huo unaohusu wananchi hao na mwekezaji aliyehodhi eneo hilo.

Wananchi hao wametishia kumnyima kura mbunge huyo katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa madai ameshindwa kuwasikiliza na kuwa, pale anapopelekewa malalamiko kuhusu mgogoro huo huyapuuza.

Kauli hiyo wameitoa leo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na uongozi wa Serikali ya Mtaa huo uliohusu kutakiwa kuondoka katika eneo hilo kwa madai kwamba, wao ni wapangaji kwa kuwa wameingia eneo hilo bila kufuata taratibu za kisheria.

Catherine Makunye, Mussa Machela, Sarah Malima na Edward John wamesema kuwa, kitendo cha John Wanga, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela kuwataka kuondoka eneo hilo kimeonesha namna serikali isivyowajali wananchi wake.

Wamesema kuwa, wakati waliponua kwa aliyekuwa enzi hizo bwana ardhi, Abdaral Amrani hawakuelezwa kama eneo hilo kuna mwekezaji lakini wanashangaa kuona serikali ikiwataka kuondoka eneo hilo.

Wamesema kuna baadhi ya wakazi wa eneo hilo lenye kaya zaidi ya 500, walianza kuishi hapo tangu mwaka 2000 lakini wanashangaa kusikia kuna mwekezaji ambaye alinunua eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa shule, kitendo ambacho wamedai ni cha unyanyasaji na kwamba, hawapo tayari kuondoka.

“Mimi nimenunua eneo hili mwaka 2000 na nilipopanunua tu, nilianza kujenga na sasa naishi eneo hili tangu kipindi hicho mpaka sasa ni miaka 17, iweje leo ndio serikali wasema kuna mwekezaji alinunua eneo hili,” amehoji Musa Machela na kuongeza;

“Huyu mwekezaji tangu mwaka jana ndio kelele hizi zimeanza, alafu mtu mwenyewe hajui hata mipaka yake, hivi karibuni ndio amekuja na watu wa ardhi ili wamuoneshe mipaka, sasa tunashangaa aliponunua hakuoneshwa hiyo mipaka?”

Wananchi hao wamesema kuwa, walinunua eneo hilo kwa bwana ardhi kwa nyakati tofauti na walikuwa wakiandikishana kwa maandishi na viongozi wa serikali ya mtaa huo hivyo wao ni wamiliki halari wa maeneo hayo.

Kiyoga Ibrahim, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji wa Mgogoro huo amesema,  mgogoro huo umesababisha mwenyekiti wa mtaa huo kubambikiziwa kesi ili asiendelee kulifuatilia suala hilo.

Ibrahim amesema kuwa, uongozi wa Manispaa ya Ilemela umekuwa ukifanya mambo bila kuwashirikisha viongozi wa mtaa huo na badala yake wamekuwa wakimpa ushirikiano mwekezaji huyo kuliko wananchi ambao ndio wahanga wakubwa kitendo ambacho walidai kuna uwezekano wa viashiria vya rushwa.

Bwana ardhi (Amrani) akizungumzia mgogoro huo amekiri kuwauzia Wananchi maeneo hayo huku akidai eneo hilo zamani lilikuwa shamba.

Amesema, alikuwa akiwauzia Wananchi kama shamba na sio kiwanja pia ameeleza kushangazwa kusikia kuna mwekezaji eneo hilo.

Amrani amesema kuwa, miaka ya 1970 eneo hilo alikuwa akilima mihogo na mazao mengine lakini hakuwahi kusikia kwamba kuna mwekezaji ambaye alinunua eneo lake na wala hajawahi kuliuza kwa mwekezaji yeyote yule.

Wankuru Maswi, mwekezaji wa eneo hilo ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Uchimbaji wa Visima vya Maji Maswi amesema, alinunua eneo hilo mwaka 2006 kutoka serikalini chini ya aliyekuwa Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Jiji la Mwanza aliyetajwa kwa jina moja la Tegambwa.

Amesema kuwa, amedai eneo hilo kwa njia halali na mpaka sasa anaendelea kulilipia kodi eneo hilo kila mwaka.

Na kwamba, Wananchi wanaoendelea kuishi eneo hilo ni wapangaji wake na muda wowote atawatimu kutoka eneo hilo.

“Eneo hilo tunataka kujenga shule, mpaka sasa tayari tumejenga nyumba nane za walimu na kilichobaki ni ujenzi wa madarasa na eneo hilo mimi nalimiliki kihalali lakini sasa hivi nashangaa kuona wananchi wakijenga na kuishi hapo,” amesema Maswi.

John Wanga, Mkurugenzi wa Ilemela alipotafutwa kuzungumzia suala hilo kupitia simu yake ya mkononi, alidai yupo safari nakuahidi akirejea ofisini kwake, atalifanyia kazi baada ya kupewa taarifa na wataalamu wa ardhi kuhusu mgogoro huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!