Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Mbunge Ditopile apongeza teuzi za Rais Samia
Habari

Mbunge Ditopile apongeza teuzi za Rais Samia

Spread the love

 

MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amempongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuteuwa mawaziri, manaibu mawaziri na makatibu wakuu ambapo wanakwenda kuboresha maisha ya Watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Akizungumza leo Jumatatu tarehe 11 Januari 2022 mbunge huyo amesema viongozi hao wapya ni wazi kuwa ni wachapakazi na wazalendo ambapo wataweza kwenda na kasi katika kutatua changamoto za wananchi.

“Rais Samia ameendelea kuthibitisha kwa vitendo anayo nia ya dhati ya kuboresha maisha ya Wananchi kwa kuteua wasaidizi wachapakazi, Wazalendo na Vijana wengi ambao binafsi naamini watakwenda speed kukimbizana na matatizo na changamoto za wananchi” amesema Mariam

Aidha, amewapongeza viongozi hao kwa kuaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo ambapo amesema kuwa “Nichukue Nafasi hii kuwapongeza Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu walioaminiwa na kuteuliwa.”

Amesema Watanzania wana imani kubwa na Serikali ya Rais Samia ambapo katika kipindi kifupi uchumi umeimarika, huduma za jamii zimeendelea kuboreshwa na kipato cha mtu mmoja mmoja kinaongezeka.

Rais Samia aliwaapisha mawaziri, naihu mawaziri na makatibu wakuu jana Jumatatu Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma , baada ya kufanya mabadiliko madogo ya mawaziri na makatibu wakuu

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!