June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CUF ataka rais awajibike

Spread the love

MBUNGE wa Kilwa Kusini kwa tiketi ya CUF, Selemani Bungara ‘Bwege’ amesema Rais John Magufuli anatakiwa kuwajibika iwapo kutatokea machafuko visiwaniZanzibar kutokana na kurudiwa uchaguzi. Anandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Alitoa kauli hiyo wakati wa mahojiaano maalumu kutokana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza kurudiwa uchaguzi wa Rais Machi 20, mwaka huu.

Bungala amesema kurudiwa kwa uchaguzi Zanzibar ni mipango ya CCM kujihakikishia ushindi.

Amesema ni ukweli usiopingika kwamba serikali inayoundwa na CCM imeamua kukanyaga demokrasia na sheria za uchaguzi na badala yake ubabe ndio unaofanyika.

“Uchaguzi huu ni batili kwani kufutwa kwa uchaguzi ilikuwa ni kinyume na sheria na katiba hata hivyo kurudiwa kwa uchaguzi tena ni kuvunja Demokrasia.

“Hawa jamaa wameshapanga ushindi na hili siyo jambo geni, CCM wamekuwa wakipora ushindi kwa maana hiyo hakuna jambo la ajabu kwani ni kawaida ya CCM kutumia mabavu.

“Hapa hakuna amani ila kuna ubabe na ikitokea kukawepo na machafuko mtu ambaye atatakiwa kushitakiwa ni rais, kwani amekaa kimya bila kutoa tamko lolote licha ya kwamba taasisi mbalimbali na vyama vya siasa kupiga kelele juu ya kutafuta ufumbuzi juu ya uchaguzi huo,” amesema Bungala.

error: Content is protected !!