Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CUF amtega Rais Magufuli
Habari za Siasa

Mbunge CUF amtega Rais Magufuli

Spread the love
MBUNGE wa Kilwa Kusini (CUF), Sulemani Bungala ameitaka serikali kuruhusu wavuvi wadogo wadogo kuendelea na shughuli zao. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni leo Jumanne, Bungala alisema, ni jambo la kusikitisha kuona serikali inaruhusu viwanda vya nyavu vinatengeneza bidhaa hiyo yenye matundu madogo na kuziuza kwa wananchi na kisha serikali kukusanya kodi.

“Mimi sielewi serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Siielewi kabisa. Yaani mimi binafsi, jamni siielewi serikali ya Rais John Pombe Magufuli. Inaruhusu viwanda vya nyavu kutengeneza nyavu zenye matundu madogo; na kisha inapokea kodi ya viwanda hivyo, lakini baadaye inashughulika na wavuvi. Siwaelewi,” alieleza Bungala.

Alisema, “Serikali ya CCM chini ya Rais Maguli, inatoa leseni kwa wavuvi, lakini ghafla inawageuka wavuvi hao hao wenye leseni na kuwanyang’anya nyavu zao na kisha kuwaita wavuvi haramu.”

Mbunge huyo ambaye anafahamika kwa jina la utani la Bwege alisema, “namtaka rais wa wanyonge, awaruhusu wavuvi hawa wa Kilwa Kusini na maeneo mengie, watumie nyavu zao, ili mradi wana leseni ya uvuvi. Maana kama wanyonge, basi wanyonge wenyewe ni wavuvi.”

Bungala alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili. Bunge limepanga kwa siku mzima ya leo, kujadili ripoti ya kamati hiyo na ile ya Kilimo, Maji na Mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!