July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CUF aichokonoa serikali

MBUNGE wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahim Sanya (CUF) akizungumza na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli

Spread the love

MBUNGE wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahim Sanya (CUF), ameitaka serikali kupiga marufuku unywaji wa pombe za kienyeji na za viwandani ili kuepuka ulevi uliopindikia nchini. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Viwanda vya pombe vilivyosajiliwa ni miongoni mwa sekta zinazoingiza kiasi kikubwa cha kodi ya mapato hivyo kuisaidia serikali kuendesha shughuli zake za maendeleo.

Mwaka 2011 kodi itokanayo na viwanda hivyo ndiyo iliyoongoza kulipa kiasi kikubwa cha fedha serikalini ambapo taasisi kubwa kama Kampuni ya Kimataifa ya Barrick inayomiliki migodi minne mikubwa ya dhahabu mkoani Mara, Shinyanga na Mwanza (Geita) haikuwemo.

Kama sivyo, Sanya ameitaka serikali kutoza kodi kwa asilimia 100 vinywaji hivyo ili kupunguza idadi ya wanywaji kwa kuwa, matumizi hayo kwa kiasi kikubwa yanachochea maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU).

Mbunge huyo pia alihoji kama kuna uwezekano wa chama kitakachoingia madarakani kwa kushinda kwa kura nyingi kuweza kutoa asilimia 10 ya ruzuku kwa ajili ya kuchangia katika mfuko wa UKIMWI kutokana  na hali ya sasa ya wafadhili kusuasua.

Sanya ametoa kauli hiyo bungeni wakati alipouliza swali la nyongeza kwa kuitaka serikali ieleze, ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wanaoishi na VVU wanapatiwa huduma muhimu za kiafya na lishe.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua serikali pamoja na kutoa huduma ya dawa kwa wanaopata Virusi vya Ukimwi,pia inawasaidiaje wagonjwa hao kwa kuwapatia lishe.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Steven Kebwe amesema, serikali haiwezi kulipa kodi mara mbili kwa kutumia ruzuku ya vyama vya siasa.

Hata hivyo amesema, serikali haiwezi kupiga marufuku pombe za viwandani isipokuwa pombe za kienyeji ndiyo inayoweza kuzuiliwa kutokana na madhara yake.

Dk. Kebwe amesema, dawa yoyote inaweza kuwa sumu iwapo itakuwa imetumiwa vibaya kwa kukiuka matumizi yaliyo stahili.

Amesema, kwa kawaida mtu ambaye anatumia pombe anatakiwa kutumia pombe isiyopitiliza na kumfanya kulewa na ikibidi kwa mwanaume anatakiwa kunywa bia tatu hadi nne kwa siku ndani ya saa 24 na kwa mwanamke bia mbili hadi 3 kwa ndani ya saa 24.

error: Content is protected !!