Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CUF adai Ripoti ya Haki za Binadamu, Utawala Bora bungeni
Habari za Siasa

Mbunge CUF adai Ripoti ya Haki za Binadamu, Utawala Bora bungeni

Spread the love

MBUNGE wa Mgogoni, Dk. Suleiman Ally Yusuph amehoji kwa nini ripoti za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania (THBUB) haziwekwi wazi kwa umma, kama inavyofanya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)? Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Yusuph amehoji hayo leo tarehe 17 Mei 2019 katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

Amesema, ni wakati sasa ripoti hizo zikawekwa wazi kwa umma, sambamba na kujadiliwa bungeni ili watu wajue changamoto zilizopo katika masuala ya haki za binadamu nchini.

“Kwa nini ripoti za tume ya haki za binadamu na utawala bora haziwekwi wazi kwa umma? na je serikali haioni kuwa ni wakati muhimu zikajadiliwa bungeni?” amehoji Yusuph.

Aidha, Dk. Suleiman amedai kwamba, ripoti za THBUB hazioneshi wazi matukio ya watu kutekwa na wasiojulikana kama inavyofanya LHCR.

Na kwamba, kama serikali haipati changamoto inavyopeleka ripoti zake za haki za binadamu katika vikao vya kimataifa, ambazo zinaonesha matokeo tofauti na zile zinafanywa na taasisi binafsi.

“LHRC inaweka wazi matukio yanayotokea nchini yakiwemo upoteaji, utekwaji na kubambikiziwa kesi. Ripoti za serikali hazibebi mambo mazito kama haya kwa nini?” amehoji Dk. Suleiman na kuongeza;

“Changamoto zipi serikali inazipata, inapokwenda kutoa ripoti zake katika vikao vya kimataifa huku kiukiwepo ripoti mbadala kinzani?”

Akijibu maswali hayo kwa Niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, William Tate Ole-Nasha, Naibu Waziri wa Elimu, amesema, si kweli kwamba THBUB haiweki wazi ripoti zake kwa umma, kwa kuwa tume hiyo ikishafanya uchunguzi wa mambo yanayohusu haki za binadamu na utawala bora, huwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Ole-Nasha amesema, THBUB ni taasisi huru ya umma na inayojitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na kwamba, hutekeleza jukumu lake la kufikisha ripoti zake katika mamlaka husika na bungeni.

“Ni kweli kwamba, ibara ya 130 ya Katiba ikisomwa pamoja na sheria namba 7 ya tume haki za binadamu na utawala bora, inaipa tume mamlaka ya kufanya uchunguzi wa mambo yote yanayohusu uvunjaji haki za binadamu,” amesema Ole-Nasha na kuongeza;

“Baada ya kufanya uchunguzi na kuthibitisha uwepo wa uvunjwaji wa haki za binadamu, itafikisha taarifa kwa mamlaka husika kwa ajili ya utekelezwaji, inatakiwa kufikisha taarifa yake kwa Bunge, imekuwa ikitimiza jukumu hilo kwa mujibu wa sheria.”

Kuhusu matokeo ya tafiti za THBUB kuhusu masuala ya haki za binadamu kutofautiana na ripoti za taasisi binafsi ikiwemo LHRC, Ole-Nasha amesema sheria za nchi hutoa uhuru kwa taasisi hizo kutoa maoni, na kwamba zinatoa ripoti jinsi wao wanavyoona.

“Ni kweli LHRC hutoa ripoti yenyewe inavyoona kuwa matukio ya haki za binadamu yakiendelea nchini, sheria zetu zinaruhusu, inatoa uhuru wa maoni hata watu binafsi kwa hiyo wanaongea mengi.

“Lakini katiba na sheria zetu inatambua hasa tume ya haki za binadamu na utawala bora na ndio imepewa fursa ya kuiskiliza malalamiko, kwa yoyote kmwenye malalamiko ya haki za binadamu na utawa la bora kupeleka,” amesema.

“Nimfahamishe changamoto kubwa kuliko zote ni upotoshaji mkubwa unaofanywa sio na taasisi bali na mmoja mmoja ikwiemo wanasiasa,. hivi karibuni serikali imechukua hatua upotoshaji unapofanywa wanasahihisha.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!