Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema hoi, akimbizwa Muhimbili
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Chadema hoi, akimbizwa Muhimbili

Spread the love

MBUNGE wa Chadema katika jimbo la Buyungu, mkoani Kigoma, Mwalimu Kasulu Bilango, yuko mahututi. Anasumbuliwa na tatizo la kujikunja kwa utumbo wake. Anaripoti Mwandishi Wetu .… (endelea).

Kufuatia hali ya mbunge huyo kuzidi kubadilika kila wakati, uongozi wa Bunge umelazimika kumsafirisha kwa ndege maalum mchana huu wa leo Jumanne, kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa uongozi wa Bunge, Mwalimu Bilago amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa siku kadhaa.

Kabla ya kusafirishwa jijini Dar es Salaam, alilazwa katika hospitali moja ya madhehebu ya dini ya kikirsito mjini hapa ambako alifanyiwa upasuaji.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John Pombe Magufuli (IJPM), mkoani Dodoma, Mwalimu Bilago, amesindikizwa na watu kadhaa wakiwamo baadhi ya wabunge wenzake na maofisa waandamizi kutoka ofisi ya Bunge.

Miongoni mwa wabunge waliofika uwanja wa ndege kumsindiza mbunge huyo, ni pamoja na mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na mbunge wa viti Maalum mkoani Dodoma, Immaculate Sware Semesi.

Wengine waliokuwapo, ni mbunge wa Viti Maalum mkoani Geita, Upendo Peneza, mbunge wa Viti Maalum kutoka Zanzibar, Mariam Msabaha na Gimbi Masaba, mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoani Simiyu.

Akizungumza kwa taabu wakati akitolewa kwenye gari la wagonjwa ili kupandishwa ndege, Mwalimu Bilago aliwataka wabunge wenzake walioko Dodoma kuendeleza kile alichokiita, “mapambano ya ukombozi wa wananchi.”

Alisema, “…nakwenda Dar es Salaam kupata matibabu. Nawaombeni sana mniombee kwa Mungu ili niweze kupona haraka. Niombeeni ili niweze kuungana nanyi mapema zaidi katika harakati hizi.”

Aliongeza, “ninawaacha hapa nikiwa na ombi moja kwenu. Endelezeni mapamba haya ya kuwakomboa wananchi na udhalimu wa CCM (Chama Cha Mapinduzi) na serikali yake hadi haki ipatikane. Msikubali kurudi nyuma.”

Akijibu kauli ya Bilago, Kubenea alisema, “ondoa shaka. Hatutakuangusha. Tutafanya kama unavyoagiza. Tutakuombea na tutaendeleza mapambano haya.”

Alisema, “nenda katibiwe Mwalimu. Sisi tutafanya pae ulipoishia. Usihofu.”

Tangu kuanza kwa mkutano huu wa Bunge, mbunge huyo wa Buyungu, amekuwa mwiba kwa serikali kutokana na uwezo wake mkuwa wa uchambuzi wa bajeti ya serikali, hasa katika suaa la elimu.

Mathalani, akichangia bajeti ya wizara ya elimu, Bilago ambaye kitaaluma ni mwalimu alieleza kwa kina sababu za wanafunzi wa shule binafsi kufaulu na shule za umma kufanya vizuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!