October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Chadema aomba kujiunga CCM

Spread the love

MBUNGE wa Momba (Chadema), David Silinde ametangaza kujiondoa ndani ya chama hicho na kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Silinde ametangaza uamuzi huo leo jioni Jummane tarehe 9 Juni 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia azimio la Bunge la kumpongeza Rais John Magufuli jinsi alivyoongoza Taifa katika mapambano ya janga la corona.

Wakati akihitimisha mchango wake, Silinde amesema, ametumia zaidi ya mwezi mmoja kutafakari hatima yake ya kisiasa na kuona chama anachokiongoza Rais Magufuli kinamfaa.

Huku akishangiliwa na wabunge wa CCM, Silinde amesema, “Baada ya kutafakari kwa muda mrefu, nikajiridhisha kwa nafsi yangu kuomba kuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.”

Baada ya kauli hiyo, wabunge wa CCM walishangilia na kuimba CCM, CCM, CCM huku Spika wa Bunge, Job Ndugai akimpongeza na kumtaka kuhama kutoka upande aliokuwa amekaa wa upinzani na ahamie kwa muda ule wa CCM na Silinde akafanya hivyo.

Silinde ametangaza uamuzi huo ikiwa ni wiki chache zimepita tangu Chadema ilipotangaza kumfukuza ndani ya chama hicho kutokana na kutofuata miongozo mbalimbali ya chama hicho.

Wengine waliofukuzwa pamoja na Silinde na majimbo yao kwenye mabano ni; Anthony Komu (Moshi Vijijini), Joseph Selasini (Rombo) na Willfred Lwakatare wa Bukoba Mjini.

Hata hivyo, wabunge hap wote wanne, waliwasilisha rufaa ya kupinga kufukuzwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ambapo mpaka sasa bado hakujatolewa kwa taarifa yoyote.

Komu na Selasini walifukuzwa Chadema wakiwa tayari wamekwisha kutangaza kujiunga na NCCR-Mageuzi mara baada ya mkutano wa Bunge la 11 kumalizika.

Lwakatare ameweka wazi, yeye atarekea katika chama chake cha zamani cha CUF.

Endelea kufuatilia MwanaHalisi Online & MwanaHALISI TV kwa habari mbalimbali

error: Content is protected !!