Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema ajibu mashambulizi ya Mwita  
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Chadema ajibu mashambulizi ya Mwita  

Spread the love

CECIL Mwambe, Mbunge Jimbo la Ndanda (Chadema) anayetajwa kwenye orodha ya wabunge wanaotaka kukimbilia CCM amesema, hajashindwa kazi. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Amesema, wale wanaohama baada ya miaka miwili au mitatu wakitumikia wananchi kwa upande wa upinzani, hawakufanya chochote hivyo wamekuwa wakitoa hoja ya kukwamishwa na chama. 

Mwambe amesema, miongoni mwa wanaotoa sababu zinazolenga kuchafua walikotoka ni aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Amesema kuwa, Waitara alikosa mwelekeo baada ya kuona siku zinakwenda na hakuna anachokifanya na kwamba, tayari aliwaambia wenzake kwamba kwa mambo yalivyo hawezi kushindwa Uchaguzi Mkuu 20120.

Aamesema kuwa, Mwita alihama baada ya kujitabiria kuwa hataweza kushinda uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2020 kutokana na kuwa na ushindani ndani ya Chadema ambapo asingeweza kushinda kwenye kura za maoni.

“Sijashindwa kazi, nafanya majukumu yangu ya kuwatumikia wananchi kama kawaida, sehemu kubwa ya ahadi zangu nimetekeleza sasa kwanini nihamu?” amehoji Mwambe na kuongeza:

“Wabunge na madiwani wanaohama upinzani na kukimbilia CCM wameshindwa kuwatumikia wananchi kwenye majimbo yao, wameona watakosa hoja ndani nan je ya chama na njia nyepesi kwao ni kuhama.”

Akizungumza na MwanaHALISI Online Mwambe amesema kuwa, wabunge wengi wamejisahau katika muda huu wa miaka mitatu, hawakutekeleza majukumu yao ndani ya majimbo yao ambapo wanaona watashindwa kwenye chaguzi kutokana na wananchi kuwachoka.

Amesema kuwa, woga wa  wabunge hao unatokana na kushindwa kutekeleza yale waliyoahidi majimboni mwao na  kwamba, hawataweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2020 kutokana na udhaifu wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!