Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema aiwakia serikali
Habari za Siasa

Mbunge Chadema aiwakia serikali

Ziwa Victoria
Spread the love

HATUA ya serikali kuahidi miradi mikubwa na kisha kuitekeleza, imemkera Gimbi Masaba, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema). Anaripoti Dandoson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Masaba ameitaka serikali kueleza ni kwanini imekuwa ikipanga kutekeleza miradi ambayo hawatekelezeki?

Akiuliza swali la nyongeza leo tarehe 3 Mei 2019 bungeni amesema kuwa, licha ya kuwa serikali imekuwa ikitoa miradi mingi mikubwa lakini haitekelezeki.

“Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria yana mabomba makubwa mawili ambapo moja lilikuwa la maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya kunywa, na bomba la pili lilikuwa la maji ya kawaida kwa ajili ya mifugo na mengineyo.

“Sasa nataka kujua mkataba huo umezingatia ufanisi wa mradi huo. Tumekuwa na miradi mingi ambayo tunayo katika bajeti ambayo hivi sasa inaelekea kuishia, sasa nataka kujua miradi ya Nyang’okolwa, Nyakabindi, Sanungu na mradi wa mhina haijatekelezwa, je mpaka lini?” amehoji.

Amsema kuwa, miradi hii bado haijatekelezeka, na kwenye kitabu cha Waziri wa Wizara ya Maji nimeona kuna miradi 10 ambayo imepelekwa Simiyu.

“Sasa nataka kufahamu, ni kwa nini serikali inatoa miradi ambayo haitekelezeki?” amehoji Masaba.

Awali, katika swali la mbunge huyo ni lini serikali itatekeleza ahadi ya kujenga mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Viktoria kuanzia Nyashimo, Ngasamo, Dutwa, Bariadi, Bariadi, Itilima, Meatu na Maswa.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kuwa, serikali serikali itahakikisha inakamilisha miradi mingi ambayo imeahidiwa.

Aidha amesema, serikali imetoa Sh. 44 Bil za kuwalipa watu ambao walitakawa kulipwa fidia zao.

aidha Awesso amesema kuwa, miradi yote ambayo imeahidiwa na serikali itatekelezwa na tatizo kubwa ilikuwa kukwama katika ulipwaji.

Na kwamba, baada ya kupata fedha za kulipa fidia, watu wanaotaka zaidi ya Sh. 44 Bil na imepatikana Sh. 5 Bil kwa ajili ya kukamilisha miradi.

Amesema kuwa, ni kweli serikali itatekeleza mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka katika Nyashimo (Busega), Bariadi, Lagangabilili, Maswa na Mwanhuzi.

Aidha Awesso alisema kuwa kwa awamu zote kutawanufaisha wananchi wapatao 834,204.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!