Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema aibukia polisi
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Chadema aibukia polisi

Susan Kiwanga, Mbunge wa Mlimba
Spread the love

MBUNGE wa Mlimba (Chadema), Suzan Kiwanga (Mama Kiwanga), pamoja na wanachama wengine 67 wa chama hicho, wameswekwa mahabusu ya kituo kikuu cha polisi mkoani Morogoro, anaandika Saed Kubenea.

Taarifa kutoka mjini Morogoro na Malinyi, wilayani Ulanga zinasema, Mama Kiwanga na wenzake wamesafirishwa kituoni hapo leo kutokea Ulanga kwa madai kuwa walichochea; na au kushiriki uchomaji moto wa ofisi ya Mtendaji Kata ya Sofi.

Viongozi hao wa Chadema, walisafirishwa kutoka Malinyi kwa kutumia magari matatu ya polisi, wamedai kupakiwa kwenye magari hayo wakiwa wamefungwa kamba mikononi kutoka mwanzo wa safari hadi mwisho.

Haikuweza kufahamika mara moja, sababu ya watuhumiwa hao kusafirishwa kutoka wilayani humo hadi Morogoro, wakati kile wanachotuhumiwa kimetokea Malinyi.

“Ni kweli kuwa hawa watu wamefikishwa hapa Morogoro na jeshi la polisi, wakiwa wamejazwa kwenye magari matatu aina ya Toyota Land cruise, wakiwa wamefungwa kamba mikononi na miguuni,” ameeleza mmoja wa mashuhuda aliyekuwapo makao makuu ya polisi mkoani Morogoro.

Naye mbunge wa Viti Maalum mkoani Morogoro, Devota Minja ameliambia gazeti hili kuwa “mbunge Kiwanga na wenzake, wameingia hapa wakiwa wamefungwa kamba na waandishi wa habari wamefukuzwa eneo la kituo cha polisi.”

Amesema, “hapa ulinzi umeimarishwa mara dufu. Waandishi wa habari wamezuiwa kuingia kwenye eneo hili na mbunge na wenzake wameripoti kupigwa sana na polisi.”

Mbunge huyo na watuhumiwa wenzake, walikamatwa juzi Jumapili na kushirikiliwa kwenye kituo cha polisi Malinyi, kabla ya kufikishwa mjini Morogoro, kwa madai ya kuchoma moto ofisi ya Mtendaji Kata.

Kwa mujibu wa jeshi la Polisi, Kiwanga na mbunge mwingine wa Chadema katika jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali, wanadaiwa kuhamisha wafuasi wa chama hicho kufanya vurugu na kuchochea uchomaji wa majengo ya umma.

Miongoni mwa majengo yanayodaiwa kuchomwa na wafuasi hao, ni Shule ya Msingi Sofi, nyumba ya walimu katika shule hiyo na ofisi ya Mtendaji wa kata ya Sofi.

Mbunge Lijualikali bado yuko machimboni, licha ya jeshi la polisi kumtaka kujisalimisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!