April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Chadema ahoji uharaka wa serikali kubinafsisha viwanda

Devotha Minja, Mbunge wa Viti Maalum Chadema

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Devotha Minja (Chadema) amehoji serikali sababu za kushindwa kufanya maandalizi mazuri katika ubinafsishaji wa viwanda? Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Na kwamba, badala yake viwanda vingi kwa sasa vimebaki kuwa sehemu za kuishi popo, mbunzi na ng’ombe.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo tarehe 2 Aprili 2019 amesema, lengo la serikali kubinafsisha viwanda ilikuwa kuboesha uzalishaji.

Na kwamba, kwa sasa kinyume chake, hivyo amehoji, ni kwanini serikali ilikuwa na uharaka wa kubinafsisha wa viwanda hivyo?

“Lengo la serikali kubinafsisha viwanda ilikuwa ni kuongeza ufasisi, kuendelea kuwepo kwa viwanda visivyofanya kazi, serikali haioni kwamba imeshindwa kutimiza wajibu wake”

“Hivi kulikuwa na uharaka gani wa serekali kubinafsisha viwanda hivyo bila kuwaandaa wawekezaji,” amehoji Minja.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua ni lini serikali itatekeleza ahadi  iliyotolewa wakati wa kampeini 2015 za kutaka kuwapatia vijana ajira?

Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara akijibu maswali hayo amesema kuwa, mpango wa serikali ni kuhakikisha viwanda vyote vilivyobinafsishwa na visivyofanya kazi vinafufuliwa ili vichangie katika uchumi na kutoa ajira kwa vijana.

Amesema, pia serikali inahamasisha ujenzi wa viwanda vipya kwa kutegemeana na fursa zinazopa nchini.

“Mkoa wa Morogoro una viwanda 14 vilivyobinafsishwa, kati ya viwanda hivyo ni viwanda nane vinavyofanya kazi na viwanda sita havifanyi kazi.

“Wizara yangu kwa kushirikiana na ofisi ya msajili wa hazina, tumefanya tathimini ya viwanda vilivyobinafsishwa nchini vikiwemo viwanda vya Mkoa wa Morogoro,” alisema Mhandisi Manyanya.

error: Content is protected !!