November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM: Serikali inatoa kipaumbele kwa wazinifu 

Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga

Spread the love

MBUNGE wa Ulanga, Goodluck Mlinga ameeleza kushangazwa na hatua ya serikali kugawa mipira ya kiume ya kujamii (kondom) kwa wazinifu bure, huku ikishindwa kugawa bure taulo za kike (pedi). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

“Mheshimiwa spika, serikali inagawa mipira ya kiume bure hadi zahanati za vijiji…, mheshimiwa spika, kweli serikali yetu inatoa kipaumbele kwa wazinifu inaacha wanafunzi, kwanini serikali isitoe pedi za kike bure kwa wanafunzi wetu?” amehoji.

Mlinga ametoa kauli hiyo baada ya kuomba mwongozo kwa Job Ndugai, Spika wa Bunge leo tarehe 22 Mei 2019.

Aliporuhusiwa na Spika Ndugai, Mlinga alianza kwa kueleza matatizo wanayokumbana nayo wanafunzi wa kike na kwa kiasi gani wanahitaji msaada wa serikali.

Ukiangalia takwimu za kufeli wanafunzi, idadi kubwa wanaofeli ni wanafunzi wa kike na wengi wanaofeli, wanatoka maeneo ya kijijini. Ukiangalia sababu kubwa ya kufeli ni kitendo chao cha kutohudhuria vizuri  masomo kipindi wanapokuwa katika siku zao za hedhi.

“Mheshimiwa spika, Bunge limekuwa likipiga kelee sana serikali namna gani itawasaidia wanafunzi kwa kuwapa pedi za bure, lakini mheshimiwa spika tumeshuhudia serikali ina utaratibu wa kutoa vifaa tiba kwa makundi mbalimbali ya wananchi wake ili kuwasaidia kuepukanan na magonjwa mbalimbali,” amesema Mlinga.

Akisisitiza hoja kuwa, watoto wa kike wanapaswa kupata msaada wa taulo za kike ni kwamba, kuna namna serikali imekuwa ikitoa msaa kutokana na azingira ya wahitajio ili kulinda afya zao.

“Katika kuboresha afya, kwa mfano mheshimiwa spika tumeona serikali inatoa ARV bure, wagonjwa wa kifafa wanapewa dawa bure, wangonjwa wa kifua kikuu (TB) wanapewa dawa bure…mheshimiwa spika serikali yetu inatoa kipaumbele kwa wazinifu inaacha wanafunzi,” amesema Mlinga.

Akijibu mwongozo huo Spika Ndugai amesema, serikali imesiki na suala hilo limezungumzwa wakati muafaka.

“Hilo nalo pia limefika serikalini na kwa wakati muafaka. Serikali itaona namna gani ya kuzungumza na Bunge kuhusiana na mambo haya,” amesema Spika Ndugai.

error: Content is protected !!