
MBUNGE wa Korogwe Vijijini (CCM), Timotheo Mnzava, anatarajiwa kuburuzwa mahakamani kesho Jumanne, tarehe 6 Julai 2021, kufuatia kuibuka kwa mgogoro katika ndoa yake na mchumba wake, Caroline Pallangyo. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa kutoka mkoani Tanga na Dodoma zinasema, anayetarajiwa kumburuza mahakamani mbunge Mzava, ni mwanamke ambaye alikuwa akiishi naye kwa miaka mitatu na kubahatika kupata mtoto, anayefahamika kwa jina la Anna.
Mbali na Mzava, wengine wanaotarajiwa kuburuzwa mahakamani, ni Caroline Pallangyo – mchumba wa Mzava, ambaye ni mtoto wa mbunge wa Arumeru Mashariki (CCM), John Pallangyo.
Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumatatu, tarehe 5 Julai 2021, kujua zaidi kuhusu sakata hili.
More Stories
Chongolo atoa siku 60 kwa MSD kupeleka vifaatiba hospitali Ushetu
NMB yafadhili wiki ya unywaji maziwa Katavi
#LIVE: Tuzo za EJAT2021, Majaliwa atoa ujumbe kwa MCT